Home Habari za michezo KUHUSU ISHU YA KUPEWA UKOCHA TAIFA STARS….NABI AANIKA MUSTAKABALI WAKE NA YANGA…

KUHUSU ISHU YA KUPEWA UKOCHA TAIFA STARS….NABI AANIKA MUSTAKABALI WAKE NA YANGA…

Habari za Yanga SC

Wakati uvumi ukienea kwamba Kocha Mkuu wa Yanga Nasreddine Nabi anawindwa kupewa kibarua Cha kuwa kocha wa Timu ya Taifa ‘Taifa Stars’ mwenyewe ametoa hatma yake.

Nabi amesema kuwa anafurahia kupewa nafasi kubwa kama hiyo ya kuifundisha Taifa Stars lakini kwasasa ni vigumu kukubali ofa hiyo.

Nabi amesema kwasasa ajira pekee ambayo anaweza kuifanya akiwa ndani ya ardhi ya Tanzania ni kuendelea kuifundisha Yanga.

“Nimeona hizo taarifa lakini hata familia yangu wameshtuka walipoona lakini niwashukuru wanaonifikiria kuhusu nafasi hiyo,”amesema Nabi.

“Naomba waambie mashabiki wa Yanga kwamba Mimi kwa hapa Tanzania kwasasa nitaifundisha timu yao pekee mpaka nitakapochukua uamuzi mwingine.

“Sina maana kwamba kuifundisha Tanzania ni kazi mbaya kwangu hapana lakini huwa Nina utaratibu wa kumaliza jambo ambalo nimelianza,ningeweza kufikiria kitu kipya kama uongozi utaniambia ajira yangu hapa imefika mwisho.

Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), linatafuta kwa haraka mrithi wa kocha Mdenish Kim Poulsen hatua ambayo imezalisha taarifa za Nabi kuhusishwa na kupewa nafasi hiyo

SOMA NA HII  BREAKING:MECHI ZOTE ZA NAMUNGO DHIDI YA WAANGOLA KUPIGWA BONGO