Home Habari za michezo HIVI NDIVYO YANGA WANAVYOITAFUTA REKODI AFRIKA….MECHI NA BAMAKO KUTOA HATMA YAO…

HIVI NDIVYO YANGA WANAVYOITAFUTA REKODI AFRIKA….MECHI NA BAMAKO KUTOA HATMA YAO…

Habari za Yanga

Matokeo ya sare ya bao 1-1, iliyoyapata Yanga Jumapili iliyopita nchini Mali mbele ya vigogo wa nchi hiyo, Real Bamako yamekuwa ya aina yake kwa Wanajangwani hao kutokana na kutengeneza rekodi mpya kwenye historia yake michuano ya CAF na kama itashinda nyumbani itaboresha zaidi.

Bao la mguu wa kushoto la Straika Fiston Mayele alilolifunga dakika ya 60 litaingia kwenye vitabu vya kumbukumbu vya Wananchi kuwa bao la kwanza kwa Yanga lililowapa sare ugenini hatua ya makundi michuano ya CAF kwa maana ya Ligi ya Mabingwa na Kombe la Shirikisho Afrika tangu mwaka 1998 iliposhiriki baada ya michuano hiyo kubadilishwa kwa mfumo wa sasa.

Aidha ni alama moja ya kwanza kwa Yanga kupata ugenini hatua ya makundi ya CAF tangu ilivyoanzishwa na kabla ya hapo ilikuwa inatoka kapa kwenye mechi zake za ugenini ikifika hatua hiyo na bao hilo la Mayele ni la kwanza kwa makundi tangu 2018 iliposhiriki mata ya mwisho.

Alama nne, ilizonazo Yanga sasa katika Kundi D ya Kombe la Shirikisho ndizo alama imekuwa ikimaliza nazo misimu mitatu ya kuingia makundi ikianza kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika 1998, kisha kurudia tena kwenye Kombe la Shirikisho Afrika 2016 na 2018 na kama itapata ushindi au sare kwenye mechi zijazo itaboresha rekodi yao ya kuvuna pointi nyingi zaidi kwenye hatua hiyo.

Msimu wa mwisho Yanga kucheza makundi ya Shirikisho ndio uliokuwa mbaya zaidi kwani timu hiyo haikufunga bao lolote ugenini, achilia mbali kupata japo pointi moja, tofauti na 1998 ilipofunga bao moja katika kipigo cha 2-1 kutoka na Asec Mimosas na 2016 ilijitutumua na kufunga mara mbili katika mechi ilizopoteza 3-1 kwa Medeama ya Ghana na TP Mazembe ya DR Congo.

Kama Yanga itafanya kweli mechi ya marudiano dhidi ya Bamako Jumatano ijayo itakuwa ni rekodi mpa kwa timu hiyo kukusanya pointi nyingi zaidi kwenye hatua hiyo, kwani itavuka zile nne ambazo ilizokuwa ikigota kwa misimu mitatu ya kucheza makundi michuano ya CAF.

Kocha wa Yanga, Nasreddine Nabi alikaririwa kabla ya kwenda Mali, kwamba kwa sasa akili yake ni kuona Yanga inapata matokeo mazuri zaidi kuliko yaliyiopo kwenye vitrabu vya kihistoria ya ushiriki wao na kwamba hawajali kama wanacheza nyumbani ama ugenini.

“Rekodi zipo ili zivunjwe, lakini tunachopambana ni kuona timu inafika mbali zaidi katika michuano hii ya Afrika, bado tuna kazi kubwa,” alikaririwa Nabi baada ya kuanza mechi kwa kipigo cha 2-0 kutoka kwa vinara wa kundi hilo, Monastir ya Tunisia kisha kuichapa Mazembe ambayo ilikuwa haijawahi kufungwa na Yanga michuano ya CAF walioikandika mabao 3-2 ndipo ikaenda kupata sare ya kwanza ugenini mbele ya Real Bamako waliochomoa dakika za majeruhi.

SOMA NA HII  ARTETA : ARSENAL BADO TUNA NDOTO ZA UBINGWA...