BAADA YA SIMBA KUTOLEWA CAF....CHAMA AANDIKA UJUMBE HUU MZITO
Habari za michezo

BAADA YA SIMBA KUTOLEWA CAF….CHAMA AANDIKA UJUMBE HUU MZITO

Marce Ben Komba April 29, 2023 4:09 pm

Mara baada ya kuondoshwa kwa cha changamoto ya mikwaju ya penalti kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika, Kiungo Mshambuliaji wa Simba SC, Clatous Chama, ameandika ujumbe mzito wakuwashukuru mashabiki.

Simba walitolewa usiku wa kuamkia Aprili 29, 2023, kwenye Robo Fainali ya Pili iliyopigwa nchini Morocco na Wydad Casablanca kufanikiwa kupata ushindi wa goli 1-0 hivyo matokeo kuwa sare baada ya mchezo wa awali Simba nao kushinda 1-0.

Baada ya kuondoshwa kwa penalti, Chama ameweka picha ya kikosi cha Simba na kuandika ujumbe huu katika ukurasa wake rasmi wa Instagram:

Imekuwa ni safari ndefu yenye mambo mengi ndani yake na hisia mchanganyiko.

Jana tulifanya kila kitu tunachokijua lakini mwisho wa siku ilibidi tukubaliane na ukweli ili tuweze kusonga mbele.

Shukrani za dhati kwa wachezaji, benchi la ufundi, Rais Mo, na mashabiki. Maombi na upendo wenu ndio umetufikisha hapa leo.

Tutachukulia matokeo ya jana kama chachu ya kuendelea kuimarika. Asanteni kwa ushauri na message zenu za kutia moyo. Mungu awabariki sana

HAKUNA ANAYEWEZA KUNIPANGIA KIKOSI CHANGU…MASHABIKI TULIENI…”NABI BAADA YA KUWASHA MOTO CAF…SHAFFIH DAUDA AFUTA KAULI…”SIMBA SIO UNDERDOG TENA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

One response to “BAADA YA SIMBA KUTOLEWA CAF….CHAMA AANDIKA UJUMBE HUU MZITO”

  1. Augustino says:

    Asanteni wachezaji wetu kazi mliyoifanya mmetuheshimisha

Leave a Reply