Uongozi wa Klabu ya Yanga SC umeanza Mchakato mapema wa kutafuta wabadala wa Mawinga wa Kimataifa wa Klabu hiyo,Tuisila Kisinda na Bernard Morrison ambapo tayari wameshawashiwa taa nyekundu za kuachana nao mara baada ya Msimu huu kumalizika.
Katika kuhakikisha wanapata Kilicho bora Yanga wamevutiwa zaidi na Winga wa Kimataifa wa Mali na Klabu ya Real Bamako, Check Oumar Diakité mwenye Umri wa Miaka 18 ambaye aliwasumbua sana kwenye Mchezo wao uliomalizika Kwa sare ya goli 1-1.
Tayari Uongozi wa Yanga umeanza Mazungumzo ya awali na kinda huyo ikiwemo kuulizia Mkataba wake na Bamako na zaidi wanataka kujiridhisha Kiwango chake atakapokuja Tanzania kucheza na Yanga ili kama watashawishiwa zaidi basi Mazungumzo na Real Bamako yataanza mapema ili kuepusha Presha huko mbeleni.
Kuna uwezekano mkubwa wa kiungo huyo kusajiliwa kwenye dirirsha kubwa lijalo haswa ukizingatia kuwa si Morrison au Kisinda ambaye ameweza kuonyesha kiwango cha kutegemewa.
Hata hivyo kusajiliwa kwa kiungo huyo kwenye kikosi cha Yanga, kutamfanya akutane na raia wenzake wa Mali akiwemo Diarra pamoja na Mammadou ambaye amesajiliwa kwenye dirisha dogo la mwezi Januari.