Fei toto Taifa Stars
Michezo

FEISAL SALUM “FEI TOTO”…MECHI NA UGANDA TUTASHINDA

Marce Ben Komba March 22, 2023 9:00 am

Kiungo wa Yanga, Feisal Salum ‘Fei Toto’ baada ya kutua nchini Misri amefunguka kwa mara ya kwanza kuhusu maandalizi ya mechi dhidi ya Uganda kufuzu Afcon 2023.

Fei Toto akihojiwa na kituo cha televisheni cha Azam amesema wamejiandaa vizuri na wanaahidi ushindi kwa watanzania.

“Kweli kuna wachezaji wapya na mwalimu mpya ila Uganda tunawaheshimu ni timu nzuri ina wachezaji wazuri, ila tutaipambania Taifa Stars ili tupate matokeo,”

Ameongeza; ” Katika mechi mbili watuombee dua na tutapata matokeo kwa uwezo wake Mungu,”

Taifa Stars itacheza mechi mbili na Uganda ikianzia ugenini Misri Machi 24 na kurudiana Machi 28 jijini Dar.

MAGAZETI: CHAMA AWEKA REKODI HAIJAWAHI TOKEA BONGO…YANGA YAPEWA NONDO MPYA SIMBA YATAMBA LIGI YA MABINGWA…YATOA WANNE KIKOSI BORA CAF…LIST KAMILI HII HAPA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply