Home CAF AHMED ALLY AWACHANA CHAMA,MANULA NA KAPOMBE…PUNGUZENI MAKOSA,TUMIENI NAFASI…AMPIGIA SALUTI KIPA VIPERS

AHMED ALLY AWACHANA CHAMA,MANULA NA KAPOMBE…PUNGUZENI MAKOSA,TUMIENI NAFASI…AMPIGIA SALUTI KIPA VIPERS

Habari za Simba SC

Uongozi wa Simba umewapa onyo mastaa wao wote wa timu hiyo kuchukua tahadhari kwenye mchezo dhidi ya Horoya unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa kwa kuwa wakifanya makosa wataadhibiwa.

Timu hiyo inayonolewa na Kocha Mkuu, Roberto Oliveira, Machi 18 inatarajiwa kushuka Uwanja wa Mkapa kumenyana na Horoya kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ya makundi ikiwa ni Kundi C.

Akizungumza nasi, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano
Simba, Ahmed Ally alisema kuwa wachezaji wote wa Simba ikiwa ni pamoja na Clatous Chama, Aishi Manula, Shomari Kapombe, Kibu Denis ni lazima waongeze umakini.

“Tunacheza na timu ambayo ikipata nafasi moja na kutufunga bao moja itarejea kujilinda ili tusipite kufikia malengo yetu, hivyo nasi lazima tuwaheshimu wapinzani wetu kwani wapo kwenye hii Ligi ya Mabingwa ambayo ni ngumu.

“Ambacho wachezaji wanapaswa ni kupunguza makosa na kutumia nafasi ambazo tutatengeneza kwani tumekuwa tukifanya hivyo mara nyingi hasa Uwanja wa Mkapa.

“Mfano wale Vipers isingekuwa uimara wa kipa wao ambaye aliokoa mashuti ya hatari saba langoni mwake basi wangefungwa zaidi ya mabao matano, lakini haikuwezekana tukapata bao moja na pointi tatu tukabaki nazo huu dhidi ya Horoya ni muhimu kushinda,”

SOMA NA HII  KOCHA YANGA AFICHUA KUMPIGA CHINI MORRISON...KUMBE ANA MAJERAHA HAYA