Home Habari za michezo HIVI NDIVYO MAYELE NA INONGA WANAVYOZIHESHIMISHA SIMBA NA YANGA NCHINI KWAKO CONGO….

HIVI NDIVYO MAYELE NA INONGA WANAVYOZIHESHIMISHA SIMBA NA YANGA NCHINI KWAKO CONGO….

Habari za Simba na Yanga

MASTAA wawili wa Simba na Yanga beki Henock Inonga na mshambuliaji Fiston Mayele wamepasua anga na sasa wamekabidhiwa msitu wa mastaa wa Ulaya kuwania namba katika kikosi cha taifa lao la DR Congo.

Inonga na Mayele mapema waliitwa katika kikosi cha awali cha DR Congo, kilichowajumuisha mastaa 42 ambapo baada ya mchujo wawili hao wamepenya na kusalia katika kikosi cha mwisho cha wachezaji 29 ambacho kimetangazwa jana na sasa watakaoingia kambini.

Inonga ambaye ni beki bora wa msimu uliopita wa Ligi Kuu Bara na staa muhimu katika ukuta wa Simba, awali alikuwa katikati ya mabeki 11 ambapo baada ya mchujo amebaki katika ukuta wa mabeki 8 waliochaguliwa na kocha Sebastian Desabre.

Inonga sasa atatakiwa kuwania nafasi akiwa na mabeki Bope Bokadi (Standard Liegge, Ubelgiji), Jodran Ikolo (Pafos FC Cyprus), Joris Kayembe (Charleroi, Ubelgiji),Chancel Mbemba (Marseille, Ufaransa), Arthur Masuaku (Besiktas, Uturuki), Gedeon Kalulu (Lorient,Ufaransa),Arsene Zola (Wydad athletic Morocco),Vital Nsimba (Bordeaux,Ufaransa).

Mayele ambaye ndio kinara wa mabao katika Ligi Kuu Bara, akifunga jumla ya mabao 15 amefanikiwa kusalia katika washambuliaji 8 wa mwisho akitoka katika 9 wa kikosi cha awali.

Mshambuliaji huyo sasa atawania namba katikakati ya washambuliaji 7 wote wanaocheza Ulaya ambao ni Cedric Bakambu (Olympiakos, Ugiriki),Silas Katompa (VFB Stuttgart,Ujerumani), Yaone Wissa (Brentford, Uingereza), Aldo Kalulu (Sochaux Ufaransa), Chadrac Akolo (Saint-Gall,Uswis), Gaetean Laura (Samsunspor ,Uturuki),Jackson Muleka (Besiktas Uturuki).

Kocha huyo Mfaransa amewajumuisha mastaa wanne pekee ambao wanaocheza Afrika wakiwemo kipa Siasi Baggio (TP Mazembe, DR Congo),Zola (Wydad Athletic), Mayele (Yanga) na Inonga (Simba) lakini Ligi ya Tanzania ndiyo pekee Afrika imetoa wachezaji wawili.

Mastaa wengi wanaocheza Ligi Kuu ya Congo wameathirika na kupoteza nafasi ya kuitwa katika kikosi cha Desabre kufuatia kusimama kwa ligi ya nchini humo kutokana na kukosekana wadhamini huku Mayele na Inonga wakinufaika kucheza mechi nyingi za ushindani za ligi na Kimataifa.

SOMA NA HII  SAKHO - TULIENI..MIMI BADO SAANNA YANI..., BARBARA NA TRY AGAIN WACHORA RAMANI YA UBINGWA CAF...