HUYU HAPA KINARA WA KADI...MECHI 17 KADI 11...UKIKUTANA NAYE PISHA NJIA
Habari za michezo

HUYU HAPA KINARA WA KADI…MECHI 17 KADI 11…UKIKUTANA NAYE PISHA NJIA

Marce Ben Komba March 17, 2023 3:58 pm

Kiungo wa Simba Saido Kanoute ndiye kinara wa kupata kadi za njano na amekuwa mchezaji wa kwanza msimu huu ndani ya Simba na ligi kuwa na kadi nyingi.

Sadio Kanoute mpaka sasa akiwa amecheza michezo 17 tayari kwenye akaunti yake amejizolea kadi kumi za njano.

Huku akiwa na kadi moja nyekundu aliyopewa kwenye mechi dhidi ya Coastal Union.

Baada ya kupewa kadi mbili za njano na akaoneshwa nyekundu, wakati Simba wakishinda mabao 3-0 kwenye mechi hiyo.

Nyota wengine wanaofuata nyayo za Kanoute ni kiungo wa Dodoma Jiji Salmin Hoza mwenye kadi za njano tisa 9 na Juma Nyosso wa Ihefu mwenye kadi za njano nane 8.

SAFARI YA KIBWANA JANGWANI KIZUNGUMKUTI…LOMALISA AUNGUZA KIBANDA…SIJUI ITAKUAJE? KAKOLANYA AFURAHIA KUITWA STARS…KUJIWEKA SAWA MUDA WOTE NI MUHIMU…HATA NIKIKAA BENCHI FRESH TU

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6131

Leave a Reply