Home Habari za Yanga ISHU NZIMA YA MKATABA WA MOLOKO HII HAPA…APINDUA MEZA KIBABE YANGA

ISHU NZIMA YA MKATABA WA MOLOKO HII HAPA…APINDUA MEZA KIBABE YANGA

ISHU NZIMA YA MKATABA WA MOLOKO HII HAPA...APINDUA MEZA KIBABE

DIRISHA kubwa la usajili lililopita winga Jesus Moloko alibakiza hatua chache kutemwa lakini kiwango alichokionyesha baada ya hapo jamaa amepindua meza na sasa yuko mezani anausoma mkataba mpya.

Yanga iko katika hatua za mwisho kusaini mkataba mwingine na Moloko baada ya kuimarika kwa kiwango chake ndani ya msimu huu akiwa winga aliyekuwa katika uwezo wa juu.

Taarifa kutoka ndani ya Yanga ni kwamba uongozi wa klabu hiyo baada ya tathimini ya kiwango chake umepokea ripoti ya benchi la ufundi, winga huyo Mkongomani anatakiwa kubaki na apewe mkataba mpya haraka.

SOKA LA BONGO linafahamu tayari uongozi wa mchezaji huyo unapitia mkataba kabla ya kusaini dili jipya.

“Tunamuongeza mkataba mpya, nadhani bila kificho ukiwatathimini mawinga wetu utaona mtu pekee aliyedumu kwa ubora hasa msimu huu ni Moloko,” alisema mmoja wa mabosi wa juu wa Yanga.

“Tumeshampa mkataba tunasubiri majibu yake na uongozi wake, nadhani amekuwa ndiye winga aliye katika kiwango bora katika mafanikio ambayo tunakwenda kuyapata msimu huu.

“Ukiacha suala la kiwango chake ripoti zinaonyesha pia hata nidhamu yake iko juu haya yote yanatusukuma kumpa kitu ambacho kitampa nguvu ya kuendelea kubaki hapa zaidi.”

Moloko raia wa Congo msimu huu hadi sasa ameshafunga mabao matatu, akiwa ana mawili kwenye ligi na moja kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika ambalo timu yake ipo hatua ya makundi.

SOMA NA HII  BAADA YA KUMALIZANA NA YANGA...SIMBA WAIGEUKIA WYDAD CA KWA HASIRA KALI