Home Habari za michezo KIUNGO SINGIDA BS…AMEANDIKA HISTORIA STARS…APATA DENI KUBWA!

KIUNGO SINGIDA BS…AMEANDIKA HISTORIA STARS…APATA DENI KUBWA!

KIUNGO SINGIDA BS...AMEANDIKA HISTORIA STARS...APATA DENI KUBWA!

Kiungo wa Singida Big Stars, Yusuf Kagoma amefunguka kuwa ni historia kwa yeye kuitwa katika kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars kwani hajawahi kuichezea timu hiyo hivyo kwake ni kitu kikubwa.

Kiungo huyo amejumuishwa katika kikosi hicho kwa mara ya kwanza kucheza mechi za kufuzu Michuano ya Mataifa ya Afrika (AFCON).

Na Tanzania ikitarajiwa kuanza mchezo wake wa kwanza dhidi ya Uganda.

Stars inatarajiwa kucheza mchezo wake wa kwanza Machi 28, mwaka huu dhidi ya Uganda kwa ajili ya kusaka tiketi ya AFCON.

Kiungo huyo alisema: “Ni historia ambayo kwangu nimeiandika katika maisha yangu kwa sababu sijawahi kuichezea timu ya Taifa ya Tanzania tangu nimezaliwa, hili ni deni kwangu kuonyesha benchi la ufundi kuwa hawajakosea kunijumuisha.

“Siwezi kusema kipaji changu ndio kimenifanya benchi la ufundi liweze kuniita kwa sababu wapo wachezaji wengi sana bora ambao naamini wanauwezo zaidi yangu, hivyo binafsi nashukuru kwa hatua┬áhii┬ámuhimu”.

SOMA NA HII  MAPEMAAA...YANGA SC YAWAPIGA MKWARA WAARABU..... "FULL HOUSE..,FULL SHANGWE WAJE TUMALIZANE"...

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here