Home Habari za michezo MANARA ASHTUKIA JAMBO YANGA…AMNYOOSHEA KIDOLE MAYELE…AONYA YA FEI TOTO…

MANARA ASHTUKIA JAMBO YANGA…AMNYOOSHEA KIDOLE MAYELE…AONYA YA FEI TOTO…

Habari za Yanga

Nyota wa kimataifa wa zamani wa Tanzania aliyewika na Yanga, Pan Africans na Taifa Stars, Sunday Manara ‘Computer’ ameshtukia jambo ndani ya kikosi cha Yanga kinachoshiriki michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika na kuitahadharisha iwe makini ili mambo yasitibuke dakika za mwishoni.

Manara ambaye ni baba mzazi wa Haji Manara ‘Bugatti’, amesema mastaa wa Yanga wanapaswa kuchukua tahadhari mbalimbali ikiwemo ya kulinda ushindi iliyopata hadi sasa kwenye mechi za Kundi D ili kumaliza vyema michezo miwili iliyosalia kukamilisha ratiba ya michuano hiyo ya CAF.

Yanga inayoshika nafasi ya pili katika msimu wa kundi hilo ikiwa na pointi saba baada ya mechi nne na imesaliwa na michezo miwili migumu, ukiwamo mmoja wa nyumbani na mwingine wa ugenini, itaanaza kuvaana na Us Monastir Machi 19 kisha kuifuata TP Mazembe Aprili 2 jijini Lubumbashi.

Manara alisema juzi mara baada ya kumalizika kwa mechi ya Yanga na AS Real Bamako ambapo vijana wa Jangwani imeshindwa 2-0 yakifungwa na Fiston Mayele na Jesus Moloko na nyota huyo wa zamani aliyekuwa Mtanzania wa kwanza kucheza soka Ulaya miaka ya 1970, alisema mastaa wa Yanga wangekuwa makini ingeshinda zaidi ya ushindi huo kwa uwezo mkubwa wa kuumiliki mpira.

Alisema timu hiyo inaipa heshima nchi ya Tanzania kutokana na kucheza vizuri huku akieeleza kwamba yeye ni mmoja wa watu wanaoikosoa Yanga inapocheza vibaya ila kwa hali ya sasa wanawapa moyo wanachama na mashabiki zake kwa kuonesha kiwango kikubwa.

“Nina imani yanga atafika robo fainali bado hatujashinda tuna mechi ngumu mbeleni muhimu kuingia na tahadhari kwasababu safari ya mpira bado ni ndefu,” alisema Manara.

Manara pia alimzungumzia kiungo Feisal Salum ‘Fei Toto’ alisema angekuwepo angeongeza kitu kwenye kikosi hicho hivyo kila mchezaji ana nafasi yake katika kikosi.

“Hivi sasa timu ishakomaa sio feisal pekee hata akitoka mayele lakini bado kungekuwa na pengo la mchezaji husika kwahiyo angekuwepo Fei Toto angeongeza nguvu.”

SOMA NA HII  MSIMU WA TUZO ZA SIMBA WARUDI KWA STAILI HII...SAFARI HII MASTAA WA KIMATAIFA WAANZA KUFUNGUA DIMBA...