Home Habari za michezo MAPYA YAIBUKA YANGA…VITA VIPYA VIMEANZISHWA…ISHU NZIMA HII HAPA

MAPYA YAIBUKA YANGA…VITA VIPYA VIMEANZISHWA…ISHU NZIMA HII HAPA

Habari za Yanga SC

Wakati mashabiki wa Yanga wakiendelea kufurahia ujio wa beki wao Ibrahim Abdullah ‘Bacca’ kuna vita mpya mbili vimeanzishwa na ‘kitasa’ hicho katika vikosi viwili tofauti.

Baada ya kuanzishwa katika mchezo wa kwanza wa hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya US Monastir, Bacca ameanzisha vita mpya vya nafasi ndani ya kikosi chake cha Yanga.

Bacca katika mchezo huo alianzishwa sambamba na nahodha wa timu hiyo, Bakari Mwamnyeto huku akionyesha kiwango bora na kuisaidia Yanga kushinda mabao 2-0 ikitinga hatua ya robo fainali ya mashindano hayo.

Kiwango hicho cha Bacca sasa kitazusha vita mpya vya nafasi ya mabeki wa kati watatu wanaopishana katika eneo hilo wakiwamo Mwamnyeto na Dickson Job.

Katika mchezo dhidi ya Monastir Kocha wa Yanga, Nasreddine Nabi aliwashtua mashabiki wa timu hiyo baada ya kumweka benchi Job na kumwanzisha Bacca kwa mara ya kwanza katika mchezo huo wa kimataifa ilhali awali alikuwa akipewa nafasi chache za kucheza mechi za Ligi Kuu Bara na Kombe la Shirikisho la Azam.

Bacca dhidi ya Monastir alionyesha ubora wa juu akidhibiti vyema mipira ya juu aliporuka dhidi ya washambuliaji wa Monastir ambapo katika miruko 11 yote, mpira alicheza yeye.

Ingawa Nabi alifurahia ubora huo wa Bacca akimsifia kwa ukomavu aliouonyesha lakini alimtaka kubaki katika kiwango chake na kuongeza ushindani kati yake na mabeki wenzake.

“Ni mtu ambaye siku zote ana kiu ya kutaka kuwa bora, tulimpa nafasi na akafanya vizuri lakini kitu muhimu hapa ni kuwa na mwendelezo wa kucheza vizuri,” alisema Nabi.

Wakati Bacca akilianzisha hivyo Yanga, vita kama hivyo pia vipo katika kikosi cha Taifa Stars ambacho katika mchezo wa wake wa kwanza dhidi ya Uganda aliendeleza makali hayo baada ya kuwa katika kikosi cha kwanza cha Taifa Stars.

Kocha Adel Amrouche katika mchezo wake wa kwanza wa Stars ugenini kuwania nafasi ya kucheza Fainali za Mataifa Afrika mwakani akitumia mfumo wa 3-5-2, alianza na Bacca na Mwamnyeto huku Job akisogezwa pembeni kulia.

Bacca pia aliaminika na kuanzishwa katika kikosi cha Stars nyumbani jana dhidi ya Uganda hali ambayo imeendelea kumhikishia nafasi beki huyo.

SOMA NA HII  KISA AUCHO KUCHEZESHWA NAFASI YAKE...MUKOKO ASHINDWA KUJIZUIA..AIBUKA NA JIPYA KUHUSU UWEZO WAKE..