Home Habari za michezo MAYELE:- YANGA TUNA KAZI YA KUFANYA…KULE MALI TULISHINDWA …

MAYELE:- YANGA TUNA KAZI YA KUFANYA…KULE MALI TULISHINDWA …

Habari za Yanga

Nyota wa Klabu ya soka ya Yanga, Fiston Mayele ameweka waz kuwa watapambana kufanya vizuri kwenye mechi zijazo za kimataifa ili kufikia malengo yao.

Timu hiyo Jumanne Februari 28 ilirejea Bongo ikitokea Mali ilipokuwa na mchezo wa Kimataifa wa Kombe la Shirikisho dhidi ya Real Bamako.

Kwenye mchezo huo ubao ulisoma Real Bamako 1-1 Yanga na kuwafanya wagawane pointi mojamoja ugenini.

Bao la Yanga lilifungwa na Mayele dakika ya 60 na kuipa pointi moja timu yake iliyokuwa na nafasi ya kupata ushindi lakini ilifungwa bao moja dakika ya 90+1 na Emile Kone.

Mayele amesema: ”Tumefanya kazi kubwa kutafuta ushindi lakini tulishindwa na sasa tuna mechi nyingine nyumbani ambazo tunahitaji kupata ushindi.

“Bado tuna nafasi ya kufanya vizuri lakini tunaomba mashabiki wazidi kuwa pamoja nasi kwa kuwa kazi bado inaendelea,”.

Mchezo ujao wa Yanga kimataifa unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa itakuwa dhidi ya Real Bamako Machi 8, 2023.

SOMA NA HII  BEKI LA YANGA..CHADRACK BOKA ASHUSHA PRESHA