Home Habari za michezo MBRAZILI WA VIPERS AINGIWA NA UBARIDI NA ‘VIBE’ LA SIMBA KWA MKAPA…APANGA...

MBRAZILI WA VIPERS AINGIWA NA UBARIDI NA ‘VIBE’ LA SIMBA KWA MKAPA…APANGA KUJA NA HILI…

Habari za Simba

Kocha Mkuu wa Mabingwa wa Soka nchini Uganda Vipers SC Roberto Luiz Bianch Pelliser amesema kikosi chake kitacheza dhidi ya Simba SC katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Barani Afrika, kikiwa na lengo la kutafuta ushindi, utakaowaweka katika nafasi nzuri kwenye msimamo wa Kundi C.

Vipers SC itacheza dhidi ya Simba SC Jumanne (Machi 07) katika Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam, ikiwa na kumbukumbu ya kupoteza mchezo uliopita kwa kukubali kichapo cha 1-0.

Kocha huyo kutoka nchini Brazil ambaye alijiunga na Vipers SC mapema mwezi Januari baada ya kuondoka kwa Kocha Robertinho aliyeibukia Simba SC, amesema anajuwa mchezo wa Jumanne utakuwa mgumu lakini amejipanga kuhakikisha wanapata ushindi.

“Ninatambua ukubwa na ugumu wa kucheza na Simba SC hasa wakiwa katika Uwanja wao wa nyumbani, lakini moja ya mikakati yangu ni kuona tunaweza kupata ushindi ili tujiweke katika nafasi nzuri na kufuzu Hatua ya Robo Fainali.”

“Tulipoteza mchezo wetu uliopita dhidi ya Simba SC tukiwa nyumbani Uganda, lakini nafasi ya kufanya vizuri ipo wazi kwetu kama Simba SC walivyofanya walipocheza ugenini, ingawa tuna jukumu kubwa la kupambana Dar es salaam.”

“Nimewasisitiza baadhi ya wachezjai wangu kuwa makini, kwa sababu Simba SC ina wachezaji wenye uzoefu na hatari, kwa hiyo tunaendelea kujiandaa na bado hatujakata tamaa ya kupambana na kumaliza katika nafasi nzuri katika kundi letu.” amesema Kocha Bianchi.

Hadi sasa Raja Casablanca ya Morocco inaongoza msimamo wa Kundi C ikiwa na alama 09, ikifuatiwa na Horoya AC ya Guinea yenye alama 04, Simba SC ipo nafasi ya tatu ikifisha alama 03 na Vipers SC ipo nafasi ya mwisho kwa kuwa na alama 01.

SOMA NA HII  WAKATI MABOSI WAKIMZUNGUSHA ZUNGUSHA...ONYANGO AILILIA 'THANK YOU' YAKE SIMBA....