Home Habari za michezo AHMED ALLY ;- IWE JUA IWE MVUA SIMBA KESHO LAZIMA KIELEWEKE….

AHMED ALLY ;- IWE JUA IWE MVUA SIMBA KESHO LAZIMA KIELEWEKE….

Habari za Simba

Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Klabu, Ahmed Ally amesema hakuna jambo jingine wanalihitaji kwenye mchezo wa kesho dhidi ya Vipers SC ya Uganda zaidi ya ushindi.

Ahmed amesema ushindi dhidi ya Vipers utaiongezea Simba nafasi ya kufuzu hatua ya robo fainali kwa kuwa watafikisha alama sita hivyo ni jukumu la Wanasimba wote kuaniza viongozi, benchi la ufundi, wachezaji mpaka mashabiki kila mmoja kutimiza wajibu wake.

“Jumanne tuna jukumu zito Wanasimba, tunahitaji kujitokeza kwa wingi uwanjani kuipa sapoti timu yetu. Ni matumanini yetu kila mmoja atatimiza majukumu yake,” alisema Ahmed.

SOMA NA HII  YANGA YENYE OKRAHA YAANZA KUOGOPWA HUKO...11 YA GAMONDI HUENDA IKAWA HIVI SASA...