Home Habari za Usajili Yanga VUTA NIKUVUTE USAJILI…AL HILAL YAWAMWAGIA MPUNGA YANGA… “HATUUZI MCHEZAJI HATUNA NJAA

VUTA NIKUVUTE USAJILI…AL HILAL YAWAMWAGIA MPUNGA YANGA… “HATUUZI MCHEZAJI HATUNA NJAA

VUTA NIKUVUTE USAJILI...AL HILAL YAWAMWAGIA MPUNGA YANGA...

Imeelezwa kuwa klabu ya Al Hilal ya Sudan inayofundishwa na kocha mwenye jina kubwa Afrika, Florent Ibenge inaangalia uwezekano wa kuipata saini ya mshambuliaji wa Yanga, Kennedy Musonda katika usajili wa msimu ujao.

Musonda ni kati ya wachezaji waliosajiliwa na Yanga katika usajili wa dirisha dogo katika msimu huu.

Taarifa ambazo tumezinyaka, Ibenge ndiye anashinikiza uongozi wa Al Hilal imsajili mshambuliaji huyo ambapo wapo tayari kutumia kitita chochote cha fedha ili kufanikisha usajili huo.

Aliongeza kuwa licha ya Al Hilal kuwepo kitita chochote cha fedha, lakini kwa upande wa uongozi hauna mpango huo, kwani wanatengeneza timu hivi sasa.

“Tayari uongozi umepewa taarifa na benchi la ufundi kuwa hivi sasa wanatengeneza timu pekee, hivyo hawatakubali kumuachia mchezaji yeyote aliyekuwa katika mipango yao.

“Hivyo kama uongozi umekubaliana kwa pamoja kupitisha maombi hayo ya kocha ya kutomuuza mchezaji aliye katika mipango na kocha.

“Haitoshi uongozi upo katika mipango ya kukisuka kikosi imara na tishio Afrika, kwa lengo la kufanya vizuri kimataifa,” alisema mtoa taarifa hiyo

hatutakubali kumuachia mchezaji yeyote aliyekatika mipango ya benchi la ufundi. Alisema Raisi Injinia Hersi Said

“Na tupo tayari kuboresha mkataba wa mchezaji ili asiondoke katika timu kama ilivyokuwa kwa baadhi ya wachezaji wetu,” alisema Hersi.

SOMA NA HII  MSHAMBULIAJI HATARI WA MADEAMA AREJEA KIKOSINI KUIMALIZA YANGA