Home Habari za michezo WACHEZAJI WAWILI WAPIGWA NA RADI WAKICHEZA MECHI…WAFARIKI HAPO HAPO

WACHEZAJI WAWILI WAPIGWA NA RADI WAKICHEZA MECHI…WAFARIKI HAPO HAPO

WACHEZAJI WAWILI WAPIGWA NA RADI WAKICHEZA MECHI...WAFARIKI HAPO HAPO

Wachezaji wawili nchini Kenya wamefariki dunia kwa kupigwa na radi walipokuwa uwanjani katika mechi ya kirafiki katika Kaunti ya Kisii.

Sammy Musa, 20, na Joshua Nyangaresi, 21, walipoteza maisha wakati wa pambano la kirafiki kati ya timu za wenyeji Manyansi FC na Nyagiti FC katika uwanja wa Manyansi eneo bunge la Kitutu Chache Kaskazini.

Wachezaji wengine wawili walijeruhiwa vibaya lakini hali zao zinaendelea vizuri baada ya kukimbizwa katika hospitali katika kaunti jirani ya Nyamira, kwa mujibu wa mwenyekiti wa Shirikisho la Soka la Kitutu Chache Kaskazini, Evans Akang’a.

“Walikuwa wakicheza huku mvua ikinyesha. Ni bahati mbaya sana kwamba walipoteza maisha wakati wakicheza mchezo ambao waliupenda zaidi. Kama maafisa wa shirikisho, tunaomba pole kwa familia zilizoathiriwa,” Bw Akang’a aliambia Nation Sport kwa simu.

Bw Akang’a alitoa wito kwa serikali kuweka vizuizi vya kuzuia umeme katika shule za msingi kwa sababu wachezaji hutumia sehemu kubwa ya viwanja vyao vya michezo.

“Hakuna sheria ya FIFA inayosema mchezo lazima usimame wakati mvua inanyesha, isipokuwa tu uwanja umejaa maji kiasi kwamba wachezaji wanapata tabu kupitisha mpira. Kwa hivyo tunaomba mamlaka zetu zihakikishe wakamataji umeme wanawekwa shuleni, makanisani na majengo mengine ili kupunguza visa hivyo kujirudia,” mwenyekiti huyo alisema

SOMA NA HII  MAYELE MCHEZAJI BORA LIGI KUU...HANA MAJIVUNO...MHOLANZI AMEFUNGUKA HAYA