Home Habari za michezo YANGA SC YAIBUKA NA HILI…YAMFUA MORISSON SPESHO KWA AJILI YA SIMBA

YANGA SC YAIBUKA NA HILI…YAMFUA MORISSON SPESHO KWA AJILI YA SIMBA

Tetesi za Usajili Bongo

Benchi la ufundi la Yanga limeanza mapema kusuka mipango ya kuicheza Kariakoo Derby itakayopigwa Aprili 16 kuanzia saa 11:00 Kwa Mkapa.

Moja na mikakati hiyo ni kumuandalia programu maalumu Bernard Morrison ili awe fiti kuimaliza Simba.

Yanga ilimwacha Morrison, jijini Dar es Salaam makusudi ili aendelee na programu maalumu ya kumfanya awe fiti zaidi baada ya kupona jeraha lake la nyonga lililomweka nje kwa zaidi ya mwezi, lakini taarifa za ndani zimeeleza mpango huo ni mkakati wa benchi la ufundi ili kumtumia kwenye mechi mbili zijazo za Yanga pamoja na ile na Kariakoo Derby.

SOMA NA HII  ALLY KAMWE AJA NA MKWARA WA 5G DHIDI YA AL AHLY