DOKTA SIMBA AZUNGUMZA HAYA...KUHUSU MAJERAHA YA KAPOMBE,KIBU NA BANDA
Habari za michezo

DOKTA SIMBA AZUNGUMZA HAYA…KUHUSU MAJERAHA YA KAPOMBE,KIBU NA BANDA

Marce Ben Komba April 4, 2023 8:18 am

Klabu ya Simba imebainisha kuwa wachezaji Shomari Kapombe na Kibu Denis ambao walipata majeraha kwenye mchezo wa kuhitimisha hatua ya makundi ya michuano ya ligi ya mabingwa dhidi ya Raja Casablanca, watafanyiwa vipimo kubaini ukubwa wa majeraha yao leo.

Kapombe na Kibu walishindwa kumaliza dakika zote tisini katika mchezo uliopigwa huko Morocco usiku wa kuamkia Jumamosi na Simba kupoteza kwa mabao 3-1.

Hata hivyo Daktari wa Simba Edwin Kagalo amewatoa hofu Wanamsimbazi kuwa uchunguzi wa awali wa majeraha ya Kapombe hayakuonekana kuwa makubwa hivyo beki huyo mahiri wa upande wa kulia anaweza kupewa mapumziko ya siku chache.

Nyota mwingine ambaye atafanyiwa vipimo ni winga Peter Banda aliyepata majeraha wakati akiwa kwenye majukumu ya timu ya Taifa.

Msimu huu haukuwa mzuri kwa Banda kwani majeraha yamekuwa changamoto kubwa kwake.

SIMBA NA YANGA ZAISHTUA AFRIKA…ZAPANDA VIWANGO VYA CAF KWA KASI YA AJABU RAGE AMPIGA TWISHENI KOCHA SIMBA…AWAFUNDISHA WACHEZAJI NA MAKOCHA… ISHU NZIMA IKO HIVI

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply