Kocha wa Simba, Roberto Oliviera ‘Robertinho’ jeuri, ndivyo unavyoweza kusema kwani licha ya kupangwa dhidi ya Wydad Casablanca ya Morocco katika hatua ya Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika ameibuka na kuchimba mkwara mzito kuwa hawajali ugumu wa changamoto hiyo na anachofahamu ni kuwa timu. yao itashinda na kufuzu hatua ya nusu fainali.
Juzi Jumatano Shirikisho la Soka Afrika (Caf) lilifanya droo ya mashindano ya kimataifa kwa maana ya Ligi ya Mabingwa Afrika na Kombe la Shirikisho Afrika ambapo Simba wamepangwa kuvaana na Wydad Casablanca.
Michezo hiyo ya robo fainali inatarajiwa kuanza kupigwa kuanzia Aprili 22, mwaka huu ambapo Simba wanatarajia kuanzia mchezo wao wa mkondo wa kwanza nyumbani kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa kabla ya kumalizia ugenini nchini Morocco.
Akizungumza nasi, Robertinho alisema: “Illikuwa droo nzuri na naweza kusema hakuna kitu kipya, tulifahamu tangu mwanzo kuwa tungekutana na timu mojawapo kati ya tatu ambazo ziliongoza katika hatua ya makundi wakiwemo Raja Casablanca.
“Tutakuwa na michezo miwili migumu dhidi ya Raja, lakini kama ambavyo nimesema mara nyingi kuwa naamini kwenye ubora wa wachezaji tulionao na narudia tunataka kucheza nusu fainali na hayo ndiyo malengo yetu na tutapamana kuhakikisha tunafanikiwa.”