Habari za Simba
Habari za michezo

MKUDE APEWA DILI NONO SIMBA…SINGIDA BS WABAKI MIDOMO WAZI

Marce Ben Komba April 8, 2023 2:40 pm

KOCHA mkuu wa Singida BS, Hans Pluijm amesema njia pekee ya kiungo Jonas Mkude kurejea kwenye ubora wake ni kwenda katika timu nyingine na kupata muda mwingi wa kucheza.

Kocha Roberto Robertinho anawapa kipaumbele Sadio Kanoute na Mzamiru Yassin na bado wanafanya vizuri.

Akizungumza na SOKA LA BONGO, Pluijm alisema; “Iwe ndani ya nchi ama nje kwake itakuwa sawa kwa sababu anahitaji muda mwingi wa kucheza, pale kwa sasa ni ngumu kucheza kwani kuna wachezaji wanaofanya vizuri katika nafasi yake.”

“Kuna wachezaji wengi Singida kwenye eneo lake kwa hiyo ni ngumu sana kusema nitamchukua, nawaheshimu wachezaji waliopo kwenye kikosi changu, namuheshimu pia Mkude,” alisema Pluijm.

Singida BS kwenye eneo la kiungo mkabaji wapo Kelvin Nashon na Yusuph Kagoma ambao wote wamesajiliwa kwenye dirisha dogo wakitoka kwenye timu ya Geita Gold. Mkude anamaliza mkataba wake msimu huu huku akiwa hapati nafasi ya kucheza kwenye kikosi cha kwanza Simba.

MAYELE HAONEKANI KAMBINI…APIGWA CHINI YANGA…ISHU NZIMA IKO HIVI KOCHA SIMBA AWAONYESHA JEURI WYDAD CA…”HAWA MBONA FRESHI TU

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply