Kocha msaidzi wa Simba SC Juma Mgunda amesema kuwa maandalizi yanakwenda vyema kwa wachezaji wake kupokea kila kitu ambacho benchi la ufundi linafundisha na wanatambua mchezo dhidi ya Yanga ni mchezo mzito ambao utaamua hatma yao ya ubingwa.
Akizungumza Mgunda amesema;
“Tunaendelea kujiandaa vizuri, kuna msemo unasema haui mwisho mpaka ifike mwisho. Kwahiyo bado tupo kwenye mbio za ubingwa, hivyo bingwa atapatikana mpaka ligi itakapotamatika mwezi wa tano”