Home Habari za michezo MESSI “BYE BYE” ANAONDOKA PSG BURE…BARCELONA WAPIGA RADA ZAO HIZI

MESSI “BYE BYE” ANAONDOKA PSG BURE…BARCELONA WAPIGA RADA ZAO HIZI

MESSI

Manchester United wameonyesha nia ya kumsaka Victor Osimhen baada ya kutuma ujumbe wa kumfuatilia mshambuliaji huyo Mnigeria mwenye umri wa miaka 24 aliyechezea klabu ya Napoli katika mechi ya Championi Ligi wiki iliyopita. (Star)

Meneja wa Celtic Ange Postecoglou ni meneja wa hivi karibuni kufikiriwa miongoni mwa watu watakaochukua kazi ya umeneja wa Chelsea , ingawa meneja wa zamani wa Tottenham Mauricio Pochettino amesalia kuwa ndiye mgaombea mkuu wa kazi hii. (Guardian)

Paris St-Germain watamuacha Lionel Messi aondoke kwa uhamisho huru wakati mkataba wake utakapoisha msimu huu huku klabu hiyo ikipanga hali yake ijayo ya kudumu zaidi kwa majina machache ya wachezaji nyota na na kutilia mkazo zaidi katika kuendeleza vipaji vya vijana . (Mirror)

Julian Nagelsmann, ambaye alijiondoa katika kinyang’anyiro cha umeneja wa Blues wiki iliyopita, ana nia ya kujiunga na Tottenham. (Bild – in German)

Newcastle wanapanga kumhamisha mshambuliaji wa Barcelona mwenye umri wa miaka 26, Mbrazili Raphinha. (Mundo Deportivo – in Spanish)

Manchester United na Liverpool zina nia ya kusaini mkataba na kiungo wa kati wa Argentina mwenye umri wa miaka 24 Alexis Mac Allister kutoka blabu ya Brighton. (Fabrizio Romano)

Aston Villa wanaangalia uwezekano wa kulipa dau la mara dufu ya pauni milioni 53 kwa ajili ya mlinzi wa Manchester City mwenye umri wa miaka 32, Muingereza Kyle Walker na kiungo wa kati wa England Kalvin Phillips, 27. (Football Insider)

Ollie Watkins amekubali mkataba mpya wa muda mrefu katika Aston Villa licha ya klabu kama vile Arsenal, Tottenham Hotspur na Newcastle United kuelezea nia ya kumsaka mshambuliaji huyu Muingereza mwenye umri wa miaka 27. (Teamtalk)

Brighton wanakaribia kusaini mkataba na mlinzi mwenye umri wa miaka 16 mzaliwa wa Uskochi Ronan Ferns kutoka klabu ya Celtic. (Football Insider)

Takriban wachezaji 10 wa Chelsea wanatazamia kuendelea kubaki katika klabu hiyo kwa siku zijazo baada ya kushindwa kwao katika mchezo wa Ligi ya Championi na Real Madrid wiki iliyiopita kumaliza matumaini yoyote ya kujaa taji la fedha na katika msimu ujao wa soka wa ulaya. (Standard)

Barcelona inawafuatilia kwa karibu wachezaji 13 huku wakiangalia uwezekano wa kusaini mkataba na mchezaji wa safu ya nyuma -kulia msimu huu, akiwemo mchezaji wa Manchester United Diogo Dalot mwenye umri wa miaka 24 na Joao Cancelo mwenye umri wa miaka 28, ambaye kwa sasa anacheza kwa mkataba wa mkopo katika klabu ya Bayern Munich kutoka Manchester City. (Mundo Deportivo – in Spanish)

Chelsea wamekubali kusaini mkataba na winga Mreno Diego Moreira mwenye umri wa miaka 16 kwa mkataba huru wakati mkataba wake katika Benfica utakapomalizika katika msimu ujao. (Record – in Portuguese)

SOMA NA HII  BAADA YA KUBANJULIWA NA YANGA JUZI....MAKI APUKUTISHA MIKONO SIMBA...ATOA TAHADHARI KWA TIMU ZA LIGI KUU...