Habari za Michezo
Habari za michezo

HUYU HAPA MTALAKA WA ACHRAF HAKIMI…MFAHAMU KIUNDANI ZAIDI

Marce Ben Komba April 24, 2023 1:40 pm

Hiba Abouk aliyeachana na mumewe Achraf Hakimi, ni mwigizaji wa Uhispania ambaye aliomba talaka baada ya aliyekuwa mumewe kushtakiwa kwa kujaribu kumbaka mwanamke wa miaka 24.

Abouk (36) alizaliwa Madrid, Uhispania ana asili ya Tunisia na Lybia pia ni mtoto wa mwisho kati ya watoto wanne wa familia ya Abouk.

Muigizaji huyo ambaye amejipatia zaidi umaarufu katika kipindi chake cha El Principe kinachorushwa katika moja ya runinga nchini Uhispania.

Pia Abouk ni mwanamitindo nyota. Mwaka 2014 alitambuliwa kama mwanamke mrembo katika Tuzo za Cosmotalian Beauty.

Abouk na aliyekuwa mumewe Hakimi walifunga ndoa mwaka 2020 na kufanikiwa kupata watoto wa kiume wawili, Amin na Naim.

Inaelezwa Abouk ana utajiri wa Dola milioni 2 sawa na Sh4.6 bilioni na endapo Hakimi angekuwa na mali angepokea Dola milioni 8.5 sawa na Sh18.7 bilioni kama ombi lake la kugawana mali na mtalaka wake huyo.

Abouk, ambaye amemzidi miaka 12 Hakimi, utajiri wake unatokana na kazi yake ya uigizaji na matangazo na vipindi vinavyoruka kwenye runinga.

Hakimi (24) ana utajiri wa Dola milioni 24, sawa na Sh56.2 bilioni ingawa asilimia 80 ya mshahara wake anaolipwa kwa mwezi unaingia moja kwa moja kwenye akaunti ya benki ya mama yake.

ULE MOSHI WAIPONZA WYDAD CAF…WASHTAKIWA NA SIMBA…KUMBE WALIRUKA NA KUINGIA VIP YANGA WAMUONGEZEA MPUNGA BEKI WAO HUYU…NI BAADA YA KUWAONYESHA MAAJABU

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply