Home Habari za michezo MASHABIKI SIMBA HAWAMTAKI CHAMA WALA SAIDO…ISHU NZIMA IKO HIVI

MASHABIKI SIMBA HAWAMTAKI CHAMA WALA SAIDO…ISHU NZIMA IKO HIVI

WAZIRI AWATANGAZIA SIMBA DAU HILI KWA KILA GOLI...WAPEWA UBALOZI HUU

Shabiki na mdau wa Yussuf Mwenda amesema kuwa japokuwa wameshinda dhidi ya Wydad Casablanca nyumbani lakini kocha Robertinho alikosea kufanya mabadiliko mapema ili kuongeza kasi ya mchezo na kufunga magoli mengi.

Kauli hiyo ya Mwenda imekuja ikiwa ni siku moja baada ya Simba kuibuka na ushindin wa bao 1-0 dhidi ya Wydad katika mchezo wa kwanza wa Robo Fainali ya Kombe la Mabingwa Afrika uliopigwa katika Dimba la Mkapa.

“Mechi ilikuwa nzuri tumeshinda lakini lawama zangu ni kwa bechi la ufundi Tulikuwa tumeshaukamata mchezo kwa nini walichelewa kufanya mabadiliko mpaka dakika za mwisho? Ni kosa hilo. Walitakiwa wamtoe Chama aingie Phiri, wamtoie Saido aingie Sakho ili tuweze kuwakimbiza na kupata ushindi, tulikuwa na nafasi ya kushinda mabao matatu ya wazi.

“Sasa hivi tunaenda ugenini, namshauri kocha, tutumie mfumo wa 6- 3-1, tuna uhakika wa kumpasua Wydad. Yaani mabeki watatu ambao ni Gadiel Michale na Mohammed Hussein Tshabalala, Shomari Kapombe na Israel Mwenda.

“Katikati ni Joash Onyango, Kenedy Juma au Mohammed Ouattara, viungo aweke anasimama Moses Phiri, Clatous Chama, Sakho na Baleke anamaliza kama mshambuliaji wa mwisho, hapo lazima tushinde.

“Nina uhakika wakitumia mfumo huo tutashinda, Simba ilishawahi kufanya hivyo. Kikubwa wasichelewe kufanya sub kwa sababu mabadiliko huzaa. Watu kama Saido umri ushamuacha alitakiwa atolewe mapema.

“Kwa wakati huu Simba imewaka iko imara, hata tajiri anayetoa pesa anasema yes, Simba inakaba yote inashambulia yote, yani inapoingia uwanjani sina hofu,” amesema Mwenda.

SOMA NA HII  KIKOSI CHA YANGA KINAZIDI KUMEGUKA.....WENGINE WAWILI KUONDOKA