Imeelezwa kuwa maofisa wa Yanga wamepata taarifa za msafara mzima wa Rivers United uliotua nchini juzi alfajiri na kuweka kambi katika moja ya hoteli kubwa hapa nchini huku wakiwa na orodha ya wachezaji wote muhimu.
Awali ilielezwa kuwa Rivers United ya nchini Nigeria, imeyumba kiuchumi, ikiwa ni siku chache kabla ya mchezo wa marudiano wa marudiano wa Kombe la Shirikisho Afrika hatua ya robo fainali.
Mchezo huo unatarajiwa kupigwa leoo Jumapili saa 1 usiku kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar.
SOKA LA BONGO, lina taarifa za maofisa hao wa Yanga ambao walianza kuwafuatilia kuanzia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) hadi katika hoteli waliyofikia.
Mmoja wa maofisa hao alisema kuwa lengo la kuwafuatilia Rivers ni kutaka kujiridhisha ukweli wa ukata walioupata timu hiyo, sambamba na idadi ya wachezaji wao wanne tegemeo wanaotajwa kuachwa Nigeria kutokana na majeraha.
Ofisa huyo alisema kuwa wamejithibitishia hakuna mchezaji yeyote aliyeachwa Nigeria, na kwamba wamekuja na kikosi chao kizima kitakachocheza mchezo huo wa marudiano.
“Hatutaingia kizembe na kujiamini kuwa tunawafunga Rivers United katika mchezo wa marudiano wa Jumapili kwani tumejua ujanja na mbinu za kutudanganya kuwa wachezaji wao wanne watakosekana kutokana na majeraha.
“Kama uongozi tulianza kuwafuatilia kuanzia uwanja wa ndege maara baada ya kushuka katika ardhi ya Tanzania na kikubwa tulitaka kujiridhisha ni kweli wana ukata? Baada ya taarifa kuzagaa timu hiyo, kushindwa kusafiri kuja nchini kutokana na ukata.
“Kikubwa tulichogundua walichokuwa wanakifanya ni kututoa mchezoni, hivyo hawajafanikiwa, kwani wachezaji hao wanne wanaotajwa kuachwa katika msafara wapo nchini na watakuwepo katika mchezo huo,” alisema ofisa huyo.