Home Azam FC AZAM FC YATOLEWA NJE USAJILI WA MCHEZAJI HUYU…WATEMWA WAO NA 200MIL ZAO

AZAM FC YATOLEWA NJE USAJILI WA MCHEZAJI HUYU…WATEMWA WAO NA 200MIL ZAO

AZAM FC YATOLEWA NJE USAJILI WA MCHEZAJI HUYU...WATEMWA WAO NA 200MIL ZAO

NAHODHA wa JKT Tanzania, Edward Songo amesema uwepo wachezaji wa kigeni Championship, umeisaidia kuipa thamani kubwa ligi hiyo na inakuwa rahisi kwao kuonekana na timu za Ligi Kuu.

Akijitolea mfano baada ya kufanya vizuri msimu uliopita ambapo alikuwa kinara wa mabao 16 na sasa ana 11 kwamba alifuatwa na Azam FC iliyokuwa inahitaji huduma yake ila alishindwana nayo.

Akizungumza na SOKA LA BONGO, Songo alisema Azam ilimwekea dau la usajili la Sh100 milioni na mshahara wa Sh.3 milioni, lakini aliona sio pesa inaoweza kumvua magangwa ya jeshi na aliamini hiyo pesa anaweza akapata mkopo serikalini kwa muda mfupi.

“Niliwaambia nahitaji Sh.250 milioni, lakini hatukufikia mwafaka, yote katika yote nilionekana kwenye Ligi ya Championship ndio maana nasema kwa sasa ina thamani kubwa na ina mashabiki;

Aliongeza “Angalau maisha ya wachezaji wanaweza wakapata kitu, kikubwa ni wao wenyewe kuipa thamani kazi zao, huwezi kufika mbali kama huiheshimu hatua uliopo.”

Alisema uthamani wa ligi hiyo ndio sababu ya uwepo wa maproo wengi wenye majina, alitolea mfano wa Singida Big Stars kabla haijapanda Ligi Kuu msimu huu, kwamba ilikuwa na mastaa kibao kama Amissi Tambwe aliyemaliza mfungaji wa pili kwa mabao 14.

“Mastaa wengi ambao walitikisa Simba na Yanga walikuwepo msimu uliopita na sasa, hiyo inaonyesha kwamba ligi hiyo inalipa, hivyo ni fursa kwa wageni kuichangamkia na kupambana kuonyesha uwezo wao,” alisema.
Mbali na hilo,

alisema anatamani kuibuka kinara wa mabao ingawa yupo nyuma ya mabao mawili kinara akiwa straika wa Kitayosce Fc, Fabrice Ngoy aliye na 13.
“Bado kuna mechi, kila mmoja akipambana kwa nafasi yake atapata anachokitaka , naamini nina nafasi ya kunyakua kiatu tena, napenda ushindani wa kazi,” alisema.

SOMA NA HII  AZAM FC WATAWEZA KUTETEA NAFASI YAO