Home Habari za michezo BAADA YA KUIMUMUNYA YANGA KAMA PIPI LEO….AHMED ALLY ATAJA UELEKEO MPYA WA...

BAADA YA KUIMUMUNYA YANGA KAMA PIPI LEO….AHMED ALLY ATAJA UELEKEO MPYA WA SIMBA…

Habari za Simba

Baada ya kumalizana na Yanga leo, Uongozi wa Simba umeweka wazi kuwa licha ya kupangwa na wapinzani wakubwa katika hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika, Wydad Casablanca hawajamaliza mwendo wa mapambano watapambana kutimiza malengo yao.

Ahmed Ally, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Simba amebainisha kuwa kwenye mashindano makubwa ni lazima wakutane na wakubwa hilo haliwapi shaka kutokana na uimara walionao.

“Ni kweli tunakutana na mpinzani mgumu ambaye ni Wydad Casablanca hilo halitupi shaka na wale wanaofikiria mwendo tumemaliza waondoe kabisa akilini kama ikitokea tumepoteza basi hatuna cha kujilaumu kwa kuwa tumepambana kiasi cha kutosha.

“Tunataka kuandika historia mpya barani Afrika kwa kumtoa Wydad Casablanca sisi Simba tunafurahi kupangwa na hawa tunaamini tunakwenda kufanya vizuri.

“Wale wanaocheka kuona tumepangiwa Wydad hilo ni juu yao, sisi tunawafuata kwa nidhamu na tunajua wapo juu ila sisi tutafanya jitihada na maandalizi mazuri kwenye mechi ili kupata matokeo na kutinga hatua ya nusu fainali.”

Mchezo wa kwanza Simba inatarajiwa kuanza Uwanja wa Mkapa Aprili 21 na ule wa pili unatarajiwa kuchezwa Morocco Aprili 28.

SOMA NA HII  MAJERAHA YA KRAMO USHIRIKINA WAHUSISHWA, KAPOMBE ATAJWA