Home Habari za michezo BEKI HUYU WA ULAYA AMKOSHA KIPA SIMBA…”KILA ATAKAPOCHEZA ANA KITU KIPYA

BEKI HUYU WA ULAYA AMKOSHA KIPA SIMBA…”KILA ATAKAPOCHEZA ANA KITU KIPYA

BEKI HUYU WA ULAYA AMKOSHA KIPA SIMBA...

KIPA wa zamani wa Simba, Kelvin Mhagama amekiri kukunwa na soka tamu lililopigwa na nyota wa Taifa Stars, Novatus Dismas anayecheza soka la kulipwa barani Ulaya akisema ni muda wa wachezaji wengine kuchangamka kwenda nje ili kupanua upeo na kama vipi wajifunze kwa kiraka chipukizi.

Novatus anayecheza nchini Ubelgiji katika klabu ya Zulte Waregem alionyesha uwezo mkubwa katika michezo miwili ya Taifa Stars dhidi ya Uganda The Cranes akicheza kama beki wa kushoto, kati na baadaye eneo la kiungo na huko kote akiupiga mwingi kiasi cha kusisimua wadau wa soka nchini.

Kocha wa Stars, Adel Amrouche alimuanzisha nafasi ya beki ya kushoto katika mechi ya kwanza iliyopigwa Misri na waliporudiana alimpanga beki ya kati sambamba na Ibrahim Abdallah ‘Bacca’ na Mhagama aliyezidakia pia Mtibwa Sugar na CDA Dodoma alisema amemfuatilia kwa ukaribu nyota huyo chipukizi na kugundua kila siku anabadilika pengine kwa kucheza kwake soka la kulipwa Ulaya.

“Kila akija kuichezea timu ya Taifa ana kitu kipya anakileta kwanza ni utulivu, napenda sana utulivu wake pili kujiamini napenda sana anavyojiamini tatu kucheza namba nyingi uwanjani. Ukicheza namba nyingi unakuwa una nafasi ya kupata nafasi ya kucheza hata klabu inasema huyu tusimwache kwa sababu akiumia mtu atatusaidia,” alisema Mhagama na kuongeza;

“Ushauri wangu kwa vijana wanaocheza kwa sasa watafute timu nje, huko watajifunza vitu vingi na kuja kulisaidia Taifa, niwaombe mawakala wachezaji wa kitanzania wawape nafasi naamini wana kitu,” alisema Mhagama aliyewahi kucheza soka la kulipwa katika klabu ya Rayon Sport ya Rwanda.

SOMA NA HII  MECHI HII YA SIMBA YAZUA GUMZO...WABADILISHIWA UWANJA