Home Habari za michezo CAF YASITISHA USAJILI YANGA…NI DILI LA BRUNO KUTUA JANGWANI…ISHU NZIMA IKO HIVI

CAF YASITISHA USAJILI YANGA…NI DILI LA BRUNO KUTUA JANGWANI…ISHU NZIMA IKO HIVI

Tetesi za Usajili Yanga SC

Mmiliki wa Singida Big Stars, amesitisha mipango ya kumuachia kiungo mshambuliaji wa timu hiyo, Mbrazili, Bruno Gomes kujiunga na Yanga baada ya kuwa na uhakika wa kucheza michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika msimu ujao.

Awali ilielezwa kuwa, Yanga ipo katika hatua za mwisho kukamilisha usajili wa kiungo huyo mwenye uwezo wa kufunga mabao ya kiufundi kupitia faulo.
Mbrazili huyo hadi huu ukiwa ni msimu wake wa kwanza kucheza Ligi Kuu Bara, amefanikiwa kufunga mabao tisa.

Mmoja wa mabosi wa Yanga, kutoka ndani ya Kamati ya Usajili, ameliambia SOKA LA BONGO kuwa, baada ya Singida Big Stars kupata uhakika wa kucheza michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika inayosimamiwa na Shirikisho la Soka Afrika (CAF), wamebadili maamuzi ya kumuuza kiungo huyo.

Bosi huyo alisema kiungo huyo anabakishwa maalum kwa ajili ya michuano hiyo ya kimataifa, kwani ni kati ya wachezaji wao tegemeo msimu ujao.
Aliongeza kuwa, mabosi wa Yanga wapo katika mipango ya kumpata kiungo mwingine anayemudu kucheza namba kumi kama alivyokuwa Gomes.

“Usajili wa Gomes umeingia ugumu kutokana na mmoja wa mabosi wa Singida Big Stars, kuzuia kuondoka hapo na kujiunga na Yanga, kwani anaamini huyo ndio tegemeo lake kimataifa.

“Kutokana na umuhimu wake katika timu hiyo, katika michuano ya kimataifa, ameona ni bora kiungo ubakie hapo kwa ajili ya kuipambania timu.

“Kama Gomes atajiunga na Yanga, basi labda huyo bosi atoe baraka zake, lakini ngumu kwake kumruhusu kuondoka hapo, kwani ndio muhimu wa timu,” alisema bosi huyo.

Gomes hivi karibuni alizungumzia hilo kwa kusema: “Sina mpango wa kuondoka Singida Big Stars, kwani ninataka kuacha rekodi ambayo haitasahaulika hapa na hivi sasa akili zangu nimezielekeza katika kumalizia michezo ya ligi.”

SOMA NA HII  KUHUSU KUFELI KWA YANGA HERSI ASEMA MANENO HAYA