Home Habari za michezo MAYELE HAONEKANI KAMBINI…APIGWA CHINI YANGA…ISHU NZIMA IKO HIVI

MAYELE HAONEKANI KAMBINI…APIGWA CHINI YANGA…ISHU NZIMA IKO HIVI

MAYELE HAONEKANI KAMBINI...APIGWA CHINI YANGA...ISHU NZIMA IKO HIVI

YANGA inavaana na Geita Gold kwenye pambano la robo fainali ya Kombe la Shirikisho nchini (ASFC) litakalopigwa leo, huku kukiwa na hatihati ya kumtumia straika kinara wa mabao wa Ligi Kuu Bara, Fiston Mayele.

Msimu huu kwenye michuano ya ASFC, hajacheza dhidi ya Kurugenzi, Rhino Rangers na ile ya Prisons aliingia dakika za jioni akapasha kidogo.

Mayele amefunga mabao 15 na matatu ya Kombe la Shirikisho Afrika ambapo timu yake imetinga robo fainali ikipangwa na Rivers United ya Nigeria mechi zitakazopigwa kati ya Aprili 23 na 30 na ikifuzu itakwenda nusu kuvaana na mshindi kati ya Marumo Gallants ya Afrika Kusini au Pyramids ya Misri katika mechi zitakazopigwa kati ya Mei 14 na 21.

Habari za uhakika kutoka kwenye kambi ya Yanga iliyorejea nchini hivi karibuni kutoka DR Congo ilipoenda kucheza na TP Mazembe na kuifunga bao 1-0 na kuongoza Kundi D la Kombe la Shirikisho Afrika, zinadai kuwa, Mayele ambaye yupo na familia yake Jijini Dar es Salaam, atalikosa pambano hilo kwani juzi soka la bongo lilishuhudia alishindwa kufanya mazoezi na wenzake na hakuwepo kwenye programu ya Kocha.

“Hajafanya mazoezi na wenzake na kuna uwezekano mdogo wa kucheza kwa kile kilichoelezwa ana uchovu kwani hajapumzika tangu alipoenda timu ya taifa na hata kwenye mechi ya Mazembe alicheza ikiwa ni saa chache tangu atokee Mauritania kuiwakilisha timu ya taifa lake,” kilisema chanzo makini cha Yanga.

Chanzo hicho kiliongeza, straika huyo anapumzishwa kwa lengo la kutafuta nguvu kwa mechi mbili ngumu za Ligi Kuu Bara dhidi ya Kagera Sugar utakaopigwa Jumanne ijayo na ule wa Kariakoo Derby dhidi ya Simba Aprili 16 kabla ya kuanza kibarua cha mechi za robo fainali za CAF dhidi ya Rivers.

Katika hatua nyingine chanzo hicho kilidokeza pia, Yanga itaivaa Geita kesho bila ya kocha mkuu, Nasreddine Nabi aliyepo Ubelgiji kwa sasa akifuatilia hati ya kusafiria baada ya awali kujaa na kumfanya ashindwe kuambatana na timu nchini DR Congo, timu ilipovaana na Mazembe.

“Kuna nafasi ndogo ya Nabi kuwahi pambano hilo, kwani bado yupo Ulaya akifuatilia hati mpya ya kusafiria baada ya awali kujaa, hivyo timu itakuwa chini ya msaidizi wake, Cedric Kaze, kama ilivyokuwa kwenye mchezo wa Lubumbashi.” Mwanaspoti limepenyezewa kuwa, kocha huyo anawindwa na Moise Katumbi ili kwenda kuijenga Mazembe iliyopoteza makali kiasi cha kung’olewa Ligi ya Mabingwa na Kombe la Shirikisho.

SOMA NA HII  MAYELE AWEKA REKODI HII MPYA...KOMBE LA SHIRIKISHO BARANI AFRIKA