Home Burudani KIDUKU :- KWA MWAKINYO NIPEWE MIEZI MINNE TU YA KUJIANDAA NIMWONYESHE KAZI…

KIDUKU :- KWA MWAKINYO NIPEWE MIEZI MINNE TU YA KUJIANDAA NIMWONYESHE KAZI…

Mwakinyo na Kiduku

Hii ni kazi, naiheshimu sana, hiyo ni kauli ya bondia Twaha ‘Kiduku’ Kassim ambaye akiwa nyumbani kwake, muda wowote ule anapima uzito, huku akisema apewe miezi minne tu kujiandaa dhidi ya Hassan Mwakinyo.

Pamoja na mambo mengine, nyumbani kwa Kiduku hapakosekani mizani kwa ajili ya kupima uzito.

“Mimi ni mnene, nikisema najiachia, naweza kupigania hata uzani wa juu.

“Kuna muda nilifika hadi kilogramu 85 (light heavy), nikasema hapana, nikakomaa hadi nimerudi kwenye super middle (Kg 76),” alisema.

Nyumbani kwake, mizani ni sehemu ya kitendea kazi na saa 24 akiamua anapima ili kuona kama amekuwa na nidhamu ya kulinda uzani wake.

Bondia huyo namba moja nchini kwenye uzani huo, aliwahi kuwa namba moja kwenye super welter (Kg 69) anaopigania Hassan Mwakinyo na miaka kadhaa nyuma alitaka kuzichapa naye, Mwakinyo akaweka ngumu.

“Ikitokea Mwakinyo akakubali, nitashusha uzito na kucheza hilo pambano, lakini nipewe miezi minne tu ya maandalizi ikiwamo kupunguza uzani,” alisema bondia huyo mwenye mikanda tisa hadi sasa ikiwamo miwili ambayo alishinda Jumamosi iliyopita alipomchapa Iago Kiziria kutoka Georgia.

SOMA NA HII  HAYA HAPA MAMBO 6 WALIYOPITISHA SIMBA LEO...NAFASI YA MANGUNGU MHHH...KABURU ATOA NENO...