Home Habari za michezo KUMBE CHANZO CHA UGOMVI KATI YA MANE NA SANE SIO UBAGUZI…UKWELI MZIMA...

KUMBE CHANZO CHA UGOMVI KATI YA MANE NA SANE SIO UBAGUZI…UKWELI MZIMA HUU HAPA…

MANE ATUPIWA VILAGO BAYERN...DUUH!! APIGWA FAINI HII...KISA KITASA ALICHOMPIGA SANE

Wakati wengi wakidhani kwamba chanzo cha ugomvi wa Mastaa wa Bayern Munich Sadio Mane na Leroy Sane pengine ni kauli za ubaguzi kutoka kwa Sane kwenda kwa mane basi utakuwa unakwenda nje ya ukweli.

Leroy Sane ni mtoto wa mchezaji wa zamani wa timu ya taifa ya Senegal, Souleyamane Sane.

Japo mama yake mzazi, Regina, ni mzungu lakini Sane na familia yake amepitia ubaguzi maisha yake yote.

Kwenye macho ya mzungu, chotara siyo mzungu na anastahili kubaguliwa tu.

Kwa maisha aliyokulia yeye, hawezi kujiona mzungu hadi kufikia kumbagua Sadio Mane.

Kilichotokea baina ya wawili hao;

Kwa mujibu wa habari kutoka Senegal ni kwamba Sane alimwambia Mane ajikaze uwanjani wakati wa mchezo wao dhidi ya Man City. Inaarifiwa kuwa Sane alimwambia Mane

‘Yaani wewe unakuwa mzuri unapoenda kununua MacDonald tu, uwanjani unalegea’.

Ni maneno haya ndiyo yaliyomkera Mane, kuanzia uwanjani hadi waliporudi vyumba vya kubadilishia nguo baada ya mchezo.

Mane alipomfuata Sane kumlalamikia kwa hiyo kauli yake, akarudia tena…”Ndiyo, unakazana ukienda MacDonald tu”.

Kilichofuata baada ya hapo ni Sane kutoka damu na Mane kusimamishwa!

SOMA NA HII  FT: YANGA 2-0 SINGIDA BIG STARS.....KWA MAKALI HAYA YA GAMONDI...SIMBA TAFUTENI SABABU MAPEMA...