Home Habari za michezo KUELEKEA MECHI NA WAARABU KESHO….MANULA NA KANOUTE WAITIA SIMBA SC TUMBO JOTO…

KUELEKEA MECHI NA WAARABU KESHO….MANULA NA KANOUTE WAITIA SIMBA SC TUMBO JOTO…

Habari za Simba leo

Huenda Simba SC ikawakosa Aishi Manula na Sadio Kanoute katika mchezo wa Mkondo wa Kwanza wa Robo Fainali Ligi ya Mabingwa Barani Afrika dhidi ya Wydad Casablanca ya Morocco, kutokana na kusumbuliwa na majeraha.

Simba SC itakuwa mwenyeji wa mchezo huo Kesho Jumamosi (April 22) katika Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam, kuanzia saa kumi jioni.

Malinda Lango Manula na Kiungo Kanoute wakikosekana katika mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Young Africans uliopijwa mwishoni mwa juma lililopita (Jumapili-April 16), ambapo Simba SC ilishinda 2-0.

Manula yupo nje ya kikosi Simba SC akisumbuliwa na majeraha ya bega, wakati Kanoute anasumbuliwa na majereha nyonga.

“Manula na Kanoute hawatakuwa sehemu ya mchezo kufuatia kuwa na majeraha, hivyo kwa taarifa za madaktari tayari zipo wazi hawataiwahi Wydad hiyo Jumamosi.” Zimeeleza taarifa kutoka kambini Simba

Hata hivyo Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba  Ahmed Ally, amesema: “Ni kweli Kanoute na Manula walipata majeraha ambayo yaliwafanya kukosa mchezo dhidi ya Young Africans, hivyo kwa sasa tunasubiri ripoti ya madaktari ili tufahamu kama watakuwa sehemu ya mchezo ujao.”

SOMA NA HII  ISHU YA MKATABA WA CHAMA NA SIMBA..... UKWELI WOTE HUU HAPA...