Home Michezo AZIZ KI AWEKA REKODI HII LIGI KUU…AMPIGA KO HII CHAMA…TAKWIMU ZOTE HIZI...

AZIZ KI AWEKA REKODI HII LIGI KUU…AMPIGA KO HII CHAMA…TAKWIMU ZOTE HIZI HAPA

Habari za Yanga leo

Kuelekea Mchezo wa kesho Jumamosi, Aprili 20, 2024 wa Dabi ya Kariakoo kati ya Yanga dhidi ya Simba, ni viungo pekee ndio wenye magoli mengi kwenye michezo ya dabi kitakwimu.Kiungo wa Yanga, Stephanie Ki Aziz amehusika kwenye magoli manne (4) kwenye mchezo wa dabi tangu alipojiunga na Yanga msimu wa mwaka 2022/23.

Takwimu za Aziz dhidi ya Simba, amecheza michezo michezo mitano akiwa amefunga mabao mawili na assists 2.Ki Aziz amehusika jumla kwenye magoli (4) kwenye michezo yote aliyokutana na Simba tangu msimu wa 2022/23 alipoanza na assist kwenye mchezo wa Ngao ya Jamii huku Yanga ikishinda 1 – 2 magoli yote ya Yanga yakifungwa na Fiston Mayele, assists ya Dickson Job na Ki Aziz.

Aziz amekuwa kiungo wa kwanza wa Ligi Kuu NBC na Yanga SC kuhusika kwenye magoli mengi kwa msimu mmoja (1) kabla Ligi haijaisha, akiwa amehusika kwenye magoli (21) mpaka sasa na amecheza michezo (18) tu.Aziz ambaye ni kinara wa upachikaji mabao kwenye Ligi hiyo mpaka sasa, amecheza michezo 18 na kulamba dakika 1,368 akiwa amefunga mabao 14 na assists 7.

Ki Aziz anaingia kesho kwenye dabi akiwa ni kiungo anayeongozakuhusika kwenye Magoli mengi kwenye mchezo wa dabi akimpiku Cloutus Chama ambaye amehusika kwenye magoli matatu (3) tangu akitane na Yanga kuanzia msimu wa 2018.

SOMA NA HII  SPORTPESA:-YANGA WAMEFANYA MAKUBWA CAF....