Home Uncategorized MICHAEL SARPONG WA YANGA AIPIGIA HESABU SIMBA

MICHAEL SARPONG WA YANGA AIPIGIA HESABU SIMBA

 


MSHAMBULIAJI wa Yanga, Mghana, Michael Sarpong amefunguka kuwa hana presha yoyote licha ya kushindwa kufunga mabao kwa kuwa anajipanga kuwaonyesha wapinzani wao Simba watakapokutana Oktoba 18, mwaka huu.

 

Sarpong ametoa kauli hiyo ikiwa safu ya ushambuliaji wa Yanga kufunga bao moja katika mechi nne za ligi msimu huu huku mabao mengine yakifungwa na beki Lamine Moro aliyetupia mawili na kiungo Tonombe Mukoko amefunga moja.

 

 Sarpong amesema kuwa kwa upande wake hawezi kuwa na presha kutokana na kushindwa kufunga mabao kwa kuwa anaamini kazi yake itaanza kuonekana katika mchezo dhidi ya watani zao, Simba.

 

“Ligi kwangu naichukulia tofauti licha ya kuwepo kwa ushindani lakini jambo kubwa ambalo nimekuwa nikiliangalia kwa sasa ni mafanikio ya timu na tumekuwa tukipambana kwa ajili hiyo.

 

“Siwezi kuwa na presha kwa sababu sifungi ila naangalia nakuwa na mchango kiasi gani kwenye timu, naamini nitakuwa sawa hata kabla ya kucheza nao na wataona kazi yangu,” amesema Sarpong.

Chanzo:Championi

SOMA NA HII  KISA WACHEZAJI HAWA WAWILI SIMBA YACHIMBA MKWARA MZITO