Home Habari za michezo MAMBO SI MAMBO KWAMSUVA….CHAMA LAKE LAZIDI KUDONDOKA VIBAYA MNOO….

MAMBO SI MAMBO KWAMSUVA….CHAMA LAKE LAZIDI KUDONDOKA VIBAYA MNOO….

Saimon Msuva

Licha ya chama lake kutokuwa salama kwenye msimamo wa Ligi Daraja la Kwanza Saudi Arabia, mshambuliaji wa Kimataifa wa Tanzania, Simon Msuva ameendelea kuwa tishio kwenye ligi hiyo kufuatia kufunga bao lake la nane msimu huu wa 2022/23.

Msuva ambaye aliukosa mchezo uliopita wa Al-Qadsiah FC baada ya wiki ya michezo ya kimataifa kutokana na changamoto ya visa, amerejea kikosini na kulisaidia chama lake kuvuna pointi moja dhidi ya Al Sahel wakiwa nyumbani, Prince Saud bin Jalawi.

Bao alilofunga kwenye mchezo huo ambao ulimalizika kwa sare ya 1-1, limemfanya kuendeleza wastani wake wa kufunga kwenye kila mchezo, akiongelea hilo na malengo ya kumaliza msimu akiwa na mabao 15, alisema,”Mchezo uliopita tulifungwa (1-0) tukiwa ugenini kwa hiyo tulitakiwa kushinda ili kusogea nafasi za juu,”

“Mipango muda mwingine sio matumizi lakini sio mbaya hata kwa pointi hii moja ambayo tumepata, nguvu zetu tunahamishia kwenye mchezo ujao ambao tutakuwa ugenini kucheza dhidi ya Al Qaisoma, inawezekana kufanya vizuri,” alisema.

Msuva ni kati ya washambuliaji wachache kwenye ligi hiyo wenye wastani wa kufunga bao moja kwenye kila mchezo, nyota huyo wa zamani wa Wydad Casablanca na Difaa El Jadida za Morocco amecheza michezo nane tu ya Ligi tangu ajiunge na Al-Qadsiah FC.

Al-Qadsiah FC ambayo ipo mchezo mmoja mbele, ipo nafasi ya 15 ikiwa na pointi 28 sawa na Najran iliyopo chini yao na ikiwa kwenye hatari ya kushuka daraja kwenye msimamo wa timu 18, waliopo juu yao wamewazidi pointi mbili tu, Jeddah.

SOMA NA HII  MAYELE AWEKA REKODI HII YANGA...APEWA JEZI YA HESHIMA...ISHU NZIMA IKO HIVI