Home Habari za michezo NGEREZA:- BALEKE SIO BORA KIVIILEEEE….INAWEZEKANA MECHI ZIJAZO AKADODA KWENYE KUFUNGA…

NGEREZA:- BALEKE SIO BORA KIVIILEEEE….INAWEZEKANA MECHI ZIJAZO AKADODA KWENYE KUFUNGA…

Habari za Simba

Mchambuzi wa masuala ya soka kupitia kituo cha Televisheni cha TV3, Alex Ngereza amekinzana na baadhi ya wachambuzi na wanahabari wenzake waliompa ‘credit’ mshambuliaji wa Simba, Jean Baleke kuwa ndiye mshambuliaji bora kwa sasa kwenye Ligi ya NBCPL.

Kauli hiyo ya Ngereza inakuja ikiwa ni siku moja baada ya Jean Baleke kuifungia Simba bao 2 kwenye mchezo wao dhidi ya Ihefu na kuisaidia timu yake kuondoka na ushindi wa bao 2-0 ugenini.

“Bado Mimi sijaamini kama mshambuliaji wa Simba, Jean Baleke ndie mshambuliaji bora kwa sasa kwenye Ligi.

“Ni kweli sasa hivi Baleke anafunga magoli ya aina zote lakini hatujui kama atakuwa na mwendelezo kiasi gani huko mbele inawezekana ikafika sehemu aka-stack kama wenzake ambao walianza kwa kasi, mwisho wakakwama,” amesema Alex Ngereza.

Baleke ambaye ni raia wa Congo DR sasa amefikisha mabao 7 kwenye Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara huku akiwa na jumla ya mabao 14 katika michezo yote ya kimashindano aliyoitumikia Simba tangu awasili kikosini hapo kwenye dirisha dogo la usajili msimu huu.

SOMA NA HII  TRY AGAIN ASHUSHA NONDO ZA MAANA SIMBA...ATANGAZA KURUDI KWA MO DEWJI...AMNYOOSHEA KIDOLE MANARA...