Home Habari za michezo MAYELE AFURAHI YANGA KUVAANA NA RIVERS…”MALENGO YETU YAMETIMIA

MAYELE AFURAHI YANGA KUVAANA NA RIVERS…”MALENGO YETU YAMETIMIA

Habari za Yanga SC

Mshambuliaji wa Yanga, Fiston Mayele amewasikia wapinzani wao watakaokutana nao katika hatua ya Robo Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika, Rivers United na kutamka haohao ndio walikuwa wanawataka, hivyo wamejileta.

Kauli hiyo imekuja mara baada ya jana usiku Shirikisho la Soka Afrika (Caf), kuchezesha droo ya Robo Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika na Yanga kuangukia kwa Rivers United ya nchini Nigeria.

Yanga wanatarajiwa kuanzia ugenini huko Nigeria kwa mujibu wa kanuni za Caf, ambazo timu inayoongoza katika kundi kwenye hatua inayofuata itaanzia ugenini na kumalizia nyumbani, Rivers United wenyewe wamemaliza katika nafasi ya pili katika kundi lao.

Akizungumza nasi, Mayele alisema kuwa kabla ya droo hiyo kuchezeshwa walijipanga kukutana na timu yoyote, lakini zaidi walitaka kukutana dhidi ya Rivers United.

Mayele alisema kuwa, malengo yao yametimia ya wao kupangwa na Rivers United, kwani wakati wakicheza michezo ya mwisho ya hatua ya makundi malengo yalikuwa ni kumaliza katika nafasi ya kwanza ili wakutane na 8mshindi wa pili wakiamini hawatapata upinzani mkubwa.

Aliongeza kuwa kukutana dhidi ya Rivers hakuwafanyi wabweteke na badala yake watatakiwa kujiandaa kwa kuwafuatilia kwa ukaribu wapinzani wao hao ili wazifahamu mbinu na wachezaji hatari wa kuwazuia watapokutana.

“Ninaheshimu ubora wa Rivers United kwani sio timu ya kuibeza kutokana na kufika katika hatua hiyo ya robo fainali ya michuano hii mikubwa Afrika.

“Licha ya ubora wao huo walionao, hautufanyi tuwaogope kwani na sisi tuna kikosi bora kitakachoipa ushindani timu yoyote tutakayokutana nao.

“Yanga tunao wachezaji wenye uzoefu na uwezo mkubwa wa kupata matokeo nyumbani na ugenini kama ilivyokuwa kwa TP Mazembe ambao wao tuliwafunga kwao na nyumbani kwetu.

“Kikubwa tunawaomba mashabiki waendelee kutusapoti katika michezo inayofuatia ya michuano hii kama walivyofanya tulivyocheza dhidi ya TP Mazembe.

“Mashabiki wetu walisafiri kwa mwendo mrefu kutoka Tanzania hadi Lubumbashi nchini Congo kuja kutusapoti, hivyo waendelee katika michezo mingine ukiwemo huu dhidi ya Rivers United tusafiri pamoja kwenda Nigeria,” alisema Mayele.

wa marudiano hivyo wanachotakiwa kufanya Simba kwa sasa nikuona wanaweza kujipanga kupata matokeo ambayo wataweza kufaidika nayo mapema,” alisema Shungu.

SOMA NA HII  "KANOUTE ANASUMBULIWA NA NYONGA...SIMBA WASHINDWA KUVUMILIA WAFUNGUKA HAYA