Home Habari za michezo MORISSON AGONGELEA MSUMALI WA MOTO YANGA…AZIZ KI AWAJIBU KIROHO MBAYA

MORISSON AGONGELEA MSUMALI WA MOTO YANGA…AZIZ KI AWAJIBU KIROHO MBAYA

MORISSON AGONGELEA MSUMALI WA MOTO YANGA...AZIZ KI AWAJIBU KIROHO MBAYA

Wananchi Yanga SC wameendelea kujikita kileleni baada ya kuwachapa Kagera Sugar bao 4-0 katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC.

Mchezo huo ambao Yanga walianza kwa kushambulia kwa kasi, walishindwa kupata matokeo kufuatia Kagera kuweka ukuta mgumu hadi kipindi cha kwanza kilipokaribia kuisha ndipo walipopata goli la penalti ambalo lilifungwa na Aziz Ki kisha baada ya kupigilia lingine la pili kabla ya kipenga cha half time kupulizwa.

Kipindi cha pili, Kagera Sugar waliamua kujilipua kwa kushambulia kwa kasi na ndipo walipompa mwanya Fiston Mayele kuweza kutupia goli la tatu kwa shambulizi la kushtukiza.

Mwishoni, Bernard Morisson ambaye aliingia kipindi cha pili, alimalizia kwa kupachika nyavuni msumari wa mwisho ambao uliwanyong’onyeza kabisa Kagera na kisha dakika za jioni kabisa, Azizi Ki akapiga mkwaju wa penalti baada ya Clement Mzize kuchezewa faulu ndani ya eneo la penalti.

Yanga imefikisha pointi 68 ikiwaacha wapinzani wao Simba SC kwa alama 8 kwani Wekundu hao wana pointi 60 wakishika nafasi ya Pili katika NBC Premier Legue.

SOMA NA HII  RAISI WA SIMBA MO DEWJI...KILA SIKU UNALALAMIKA HASARA... KAMA UMEOCHOKA ACHIA TIMU