Home Habari za michezo RASMI LIONEL MESSI AREJEA BARCELONA…ISHU NZIMA A-Z HII HAPA

RASMI LIONEL MESSI AREJEA BARCELONA…ISHU NZIMA A-Z HII HAPA

RASMI LIONEL MESSI AREJEA BARCELONA...ISHU NZIMA A-Z HII HAPA

Tetesi za Mshambuliaji wa PSG, Lionel Messi kurejea tena kwenye Klabu yake ya zamani ya Barcelona zimezidi kushika kasi baada ya nyota huyo kusafiri na familia yake hadi jijini Barcelona.

Safari ya Messi haikutarajiwa na wengi akiwa na mkewe, Antonela Roccuzzo na watoto wake walipowasili Barcelona tangu Jumamosi na kuzua minong’ono juu ya staa huyo kurejea tena Catalonia.

Vyanzo vya kuaminika vimedai kuwa mchezaji huyo wa Argentina ameonekana akiwa na mabegi 15 jambo ambalo sio la kawaida na kuchochea uvumi wa kurejea Barcelona.

Mkataba wa Messi na PSG unatarajiwa kufikia tamati Juni 30, na lengo kuu la ni kuona wanafanikiwa kumrejesha mchezaji huyo.

SOMA NA HII  KUHUSU KIPOGO CHA SHABIKI WA YANGA, UONGOZI WACHUKUA MAAMUZI HAYA