Home Habari za michezo HATIMAYE NABI AFUNGUKA…SIRI YA KUWANYUKA RIVERS UNITED…”HATUJAJA KUPIGA PICHA

HATIMAYE NABI AFUNGUKA…SIRI YA KUWANYUKA RIVERS UNITED…”HATUJAJA KUPIGA PICHA

HATIMAYE NABI AFUNGUKA...SIRI YA KUWANYUKA RIVERS UNITED...

Kocha Mkuu wa Yanga, Nasreddine Mohamed Nabi amesema kuwa mchezo wao dhidi ya wapinzani wao, Rivers United ya Nigeria
haujamalizika kwani bado kuna dakika nyingine 90 kwenye Dimba la Mkapa.

Kauli hiyo ya Nabi imekuja wakati akihojiwa na vyombo vya habari nchini Nigeria baada ya kumalizika kwa mchezo wao wa kwanza wa Robo Fainali ya Kombe la Shirikisho jana Jumapili, Aprili 23, 2023, ambapo Yanga iliibuka na ushindi wa bao 2-0, katika Dimba la Godswill Akpabio, mabao yote yakifungwa na Fiston Mayele dakika ya 73 na 81.

“Sisi hatujaja hapa kujifurahisha, nazifahamu timu za Nigeria, kupata matokeo Nigeria ni vigumu sana, lakini tupo serious na mashindano haya. Siku zote nimekuwa nikiwaambia wachezaji wangu wajitahidi kupata matokeo mazuri ugenini kabla ya kuwaza matokeo ya uwanja wa nyumbani, ndicho hicho nilichokifanya.

“Rivers ni timu nzuri, mashindano ya Klabu Bingwa mwaka 2021/22, Rivers walituondoa katika hatua za awali, kulikuwa na sababu nyingi lakini zaidi timu yetu haikuwa kwenye ubora tulionqo sasa hivi. Sasa hivi kikosi kipo imara na tupo tayari kupambana.

“Sisi Waafrika tunajuana, mechi hii haijaisha, bado kuna mechi nyingine ya marudiano kwa Mkapa baada ya siku saba, kikao changu cha kwanza na wachezaji wangu itakuwa ni kuwasisitiza hilo. Nawaheshimu Rivers, kocha na wachezaji wao wote ni wazuri, lakini sisi tuna malengo ya kufika mbali zaidi kwenye mashindano haya,” amesema Nabi.

SOMA NA HII  PAMOJA NA HALI DUNI WALIYONAYO...ZALAN FC WAAPA KUFA NA YANGA CAF...KOCHA WAO AFUNGUKA KWA UCHUNGU...