Home Habari za michezo AHMED ALLY:- TULIPOFELI NA KUANGUKA NI PALE TULIPOSAJILI WATU TULIOWAAMINI…

AHMED ALLY:- TULIPOFELI NA KUANGUKA NI PALE TULIPOSAJILI WATU TULIOWAAMINI…

Ahmed Ally Simba SC

Wakati Simba SC ikitajwa kuwa katika mpango wa Usajili, huku baadhi ya majina ya Wachezaji watakaosajiliwa yakifika mezani kwa viongozi wa Klabu hiyo, Meneja Habari na Mawasiliano Simba Ahmed Ally amesema bado hafahamu majina ya wachezaji watakaosajiliwa, lakini akasisitiza usajili watakaofanya utakuwa wa kishindo kutokana na kufanya vibaya kwenye michuano yote msimu huu.

Simba SC msimu huu 2022/23 imeshindwa kuchukua Kombe lolote baada ya kutolewa kwenye Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Barani Afrika kabla ya kutupwa nje pia katika hatua ya Nusu Fainali Kombe Shirikisho Tanzania Bara ‘ASFC’ huku matumaini ya ubingwa wa Ligi Kuu yakitoweka kutokana na kuzidiwa alama saba na watani wao wa jadi, Young Africans.

Ahmed Ally amesema: “Bado sijapewa taarifa za majina ingawa ni kweli mchakato wa usajili utaanza mapema na utakuwa wa kishindo kutokana na jinsi msimu huu ullivyokuwa mbaya kwetu, tumemaliza msimu salama licha ya kuwapo kwa mechi tatu na tutashiriki vema na kumaliza msimu vizuri kwa heshima.

“Kila shabiki anaumizwa na matokeo ya Simba SC msimu huu, tunaheshimu maumivu ya kila Mwanasimba, kikubwa ni kuangalia msimu huu na kujipanga kwa msimu ujao, kukosa ubingwa mfululizo si la kuogopesha, kuna timu nyingine nje ambazo zilikuwa na mafanikio, kwetu ni somo kwa Wanasimba kujipanga kwa ajili ya msimu ujao na kuboresha kikosi,” amesema Ahmed.

Ameongeza anaungana na mashabiki wanaotaka viongozi kufanya usajili bora, kwani mafanikio ya mpira unajikita katika usajili na hilo limewafanya msimu huu kushindwa kufikia malengo yao.

“Tulipofeli na kuanguka ni pale tuliposajili watu ambao tulitegemea watafanya vizuri, hatimaye haikuwa hivyo na tunaelekea katika usajili na viongozi wanatakiwa kuwa makini kwenye usajili kwa kuboresha kikosi kwa msimu ujao,” amesema Ahmed

SOMA NA HII  PAMOJA NA KUTOPOTEZA MECHI YOYOTE...YANGA WAKUSUDIA KUFANYA MAAMUZI HAYA MAGUMU..MWANYETO ATAJWA..