Habari za Simba SC
Habari za michezo

KISA CAF SUPER LEAGUE…SIMBA SC WAPANGA KUINGIA ‘MSITUNI’ UPYA…MASTAA WAPYA KUSHUSHWA…

admin May 11, 2023 5:35 pm

Afisa Mtendaji Mkuu wa Simba SC, Imani Kajula amesema wamejipanga kufanya usajili mkubwa baada ya kushindwa kufanya vizuri msimu huu kwa lengo la kuboresha kikosi hicho kinachotarajia kushiriki michuano ya CAF Super League.

Simba SC ni klabu pekee kutoka Ukanda wa Afrika Mashariki, itakayoshiriki michuano hiyo mikubwa Afrika ambayo inatarajiwa kuanza mwezi Oktoba mwaka huu.

Kajula amesema: “Akili na nguvu zetu ni kuboresha kikosi kwa ajili ya Super League, Simba ni miongoni timu nane katika Bara la Afrika itakayoshiriki michuano hiyo, lazima tufanye usajili mzuri kwa kuboresha kikosi chetu, sasa tunafanya kazi kwa vitendo na si maneno.

“Tumeona msimu huu hatukufanya vizuri, tumeona tatizo la kufanyiwa kazi haraka, tunakutana na mkuu wa benchi la ufundi kwa ajili ya tathmini ya kikosi na mwenendo wa msimu huu na kujadili msimu ujao,”

Klabu nyingine zitakazoshiriki Michuano ya CAF Super League ni Mamelodi Sundowns, (Afrika Kusini), Petro de Luanda (Angola), TP Mazembe (DR Congo), Horoya AC (Guinea), Wydad Atheltic Club (Morocco), Simba SC (Tanzania) and Esperance de Tunis (Tunisia) na Al Ahly (Misri).

KUHUSU ISHU YA KUOMBA KUSEPA…KUMBE SIO ONYANGO TU….MASTAA WENGI SIMBA HAWANA FURAHA… ILI KUFUZU FAINAL CAF..GSM AFANYA KUFRU YA FUNGA KAZI YANGA…MZIGO ALIOWEKA MO DEWJI HAWEZI…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply