Home Habari za michezo WAKATI JOHORA AKIPEWA ‘TALAKA’…YANGA ‘WAMUOA’ JUMLA JUMLA METACHA…

WAKATI JOHORA AKIPEWA ‘TALAKA’…YANGA ‘WAMUOA’ JUMLA JUMLA METACHA…

Habari za Yanga SC

Mabosi wa Yanga wajanja sana, baada ya kuamua kumuongezea mkataba wa miaka miwili kipa, Metacha Mnata kutokana na kuridhishwa na uwezo aliouonyesha na kumvutia kipa Nasreddine Nabi kumuamini kikosini, lakini hatua hiyo inaelezwa imefungua mlango wa kutoka kwa Erick Johola.

Metacha alijiunga na Yanga kwa mkopo wa miezi sita katika dirisha dogo la usajili la msimu huu akitokea Singida Big Stars (SBS) uliotarajiwa kumalizika mwishoni mwa msimu huu.

Chanzo cha kuaminika kutoka ndani ya Yanga, kimesema kipa huyo ataendelea kuwepo Jangwani, ili kuchukua nafasi ya Johola anayetemwa baada ya kushindwa kufanya maajabu tangu asajiliwe msimu uliopita akitokea Aigle Noir ya Burundi.

“Abutwalib Mshery bado anaendelea na matibabu, ila kuna asilimia kubwa kurudi msimu ujao, hivyo tutakuwa na makipa watatu wote wenye ushindani, lakini kwa Johola hana nafasi tena ndani ya kikosi cha Yanga,” kilisema chanzo hicho cha habari na kuongeza;

“Uongozi umeshamalizana na Metacha anachosubiri ni kumalizia ratiba kwa kumaliza msimu, hivyo yeye, Djigui Diarra na Mshery hilo ndio pendekezo la benchi la ufundi.”

Chanzo hicho, kilisema wameamua kumalizana na kipa huyo ili kuendelea kumtumia kipindi hiki ambacho timu imekosa huduma ya Mshery anayeajiunguza majeraha aliyoyapata katikati ya msimu.

“Kuna Johora, alishindwa kumshawishi kocha, ndipo ikaamuliwa kuchukua uamuzi katikati ya msimu kufanya usajili wa miezi sita uliolipa sasa mchezaji huyo ataendelea kusalia ndani ya timu.” kilisema chanzo hicho.

Aidha  baadhi ya majina ya watakaotemwa sambamba na Johola au kutolewa kwa mkopo ni David Bryson, Denis Nkane, Dickson Ambundo anayetajwa kurudi Dodoma Jiji kwa mkopo na Crispin Ngushi.

SOMA NA HII  LICHA YA UBUTU WA SAFU ZA USHAMBULIAJI YANGA, GAMONDI AFUNGUKA SOKA LAKE HILI