Home news YANGA WAIKIMBIZA SIMBA KIMATAIFA…REKODI MPYA ZAIPAISHA ANGA ZA WAARABU…

YANGA WAIKIMBIZA SIMBA KIMATAIFA…REKODI MPYA ZAIPAISHA ANGA ZA WAARABU…

Yanga SC na Simba SC

Shirikisho la Kimataifa la Historia na Takwimu za mpira wa Miguu (IFFHS) limetoa orodha ya viwango bora kwa kipindi cha Mei 1, 2022 hadi Aprili 30, 2023 ambapo timu mbili za Tanzania zimeingia 10 bora.

Mabingwa wapya wa Ligi Kuu Bara, Young Africans SC wanashika nafasi ya 9 Afrika na 104 duniani huku Simba ikishika nafasi ya 10 Afrika na 105 duniani.

Klabu ya Al Ahly ya Misri inashika namba moja Afrika huku ikiwa klabu ya kwanza kutoka Afrika kuingia ndani ya 5 bora Duniani ikiwa nafasi ya tano Duniani huku Wydad Casablanca ikishika nafasi ya pili Afrika na ya 30 Duniani.

Zamalek SC ya Misri inashika namba tatu Afrika na 47 Dunia huku Pyramids FC pia ya Misri ikishika nafasi ya 4 Afrika na ya 59 Duniani.

FAR Rabat ya Morocco inakamilisha 5 bora Afrika huku ikikamata nafasi ya 85 Duniani. Mamelodi Sundowns, Future FC ya Misri na Al Hilal Omdurman ya Sudan zinashika nafasi ya sita, saba na nane mtawalia.

SOMA NA HII  KISA MECHI NA AZAM...UONGOZI YANGA WAACHUKUA MAAMUZI MAGUMU...WACHEZAJI WATAJWA