Home Habari za michezo KISA MAFANIKIO YA YANGA CAF…TRY AGAIN NAYE ASHINDWA KUJIFICHA AISEE….’ATAPIKA’ YA MOYONI…

KISA MAFANIKIO YA YANGA CAF…TRY AGAIN NAYE ASHINDWA KUJIFICHA AISEE….’ATAPIKA’ YA MOYONI…

Habari za Simba leo

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa klabu ya Simba, Salim Abdallah ‘Try Again’, amewapongeza watani zao Yanga kwa kufika fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika n akusema mafanikio hayo yamewapa somo.

Kiongozi huyo amesema somo ambalo wamelipata kwenye mafanikio ya Yanga ni kusajili wachezaji bora wenye uwezo na uzoefu wa mashindano ya kimataifa na tayari wameuanza mchakato huo.

“Tumedhamiria kufanya usajili wa nguvu utakaokirudisha kikosi chetu kwenye ubora wa juu msimu ujao na hilo linawezekana kutokana na malengo tuliyokuwa nayo ya kuifanya Simba kuwa klabu kubwa Afrika,” amesema Try Again.

Yanga imetinga Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika, baada ya kuifunga timu ya Marumo Gallants ya Afrika Kusini mabao 2-1, na kufanya miamba hiyo ya Tanzania kusonga mbele kwa ushindi wa jumla wa mabao 4-1, hiyo ni kutokana na ushindi wa mabao 2-0 iliyoupata kwenye mchezo wa awali uliopigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.

SOMA NA HII  TFF YATOA TAMKO KUHUSU ISHU YA UCHAGUZI, ATHARI ZAKE NI KUFUNGIWA

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here