Home Habari za michezo SIKU CHACHE BAADA YA KUPATA DILI ULAYA…OPPA AFUNGUKA ISHU YA KURUDI ZAKE...

SIKU CHACHE BAADA YA KUPATA DILI ULAYA…OPPA AFUNGUKA ISHU YA KURUDI ZAKE BONGO..

Habari za Michezo Bongo

Muda wowote kuanzia sasa mshambuliaji wa Kimataifa wa Tanzania anayecheza katika klabu ya Beskitas ya Ligi Kuu Uturuki Opah Clement atarejea Bongo baada ya ligi yao kumalizika.

Opah alicheza mechi yake ya mwisho ya ligi kwa msimu huu juzi na kushuhudia timu yake ikipoteza kwa mabao 3-0 dhidi ya ALG Spor.

Opah alisema, atarejea nyumbani kupumzika akisubiri msimu mpya wa ligi ambao unatarajia kurejea mwishoni mwa mwaka huu.

Opah aliondoka Simba Queens akiwa amefunga mabao 9, lakini akiwa Uturuki hajapata muda mrefu wa kukaa uwanjani na kuitumikia timu yake.

SOMA NA HII  JEMEDARI SAID: INAKERA...YANGA WAKISHINDA WAMENUNUA MECHI... ILA SIMBA NI SAWA..?