Home Habari za michezo WAARABU WATENGA DONGE NONO KWA NABI, IBENGE ….YANGA WAJIPANGE KUPINDUA MEZA…

WAARABU WATENGA DONGE NONO KWA NABI, IBENGE ….YANGA WAJIPANGE KUPINDUA MEZA…

Habari za Yanga

Uuongozi wa Esperance de Tunis kupitia kwa Mwenyekiti wao Hamdi Maddeb umeanza mchakato wa kuinasa sahihi ya Kocha Mkuu wa Al Hilal Omdurman, Florent Ibenge ili aje kuchukua nafasi ya Kocha wao Mkuu aliyejiuzulu hivi karibuni naada ya kupooea kichapo cha (3-0) kutoka kwa Al Ahly wakiwa kwao Tunis.

Pia katika orodha hiyo ya makocha wanaohitajika na Esperance Tunis yapo majina ya makocha wengine akiwemo Pitso Mosimane na Nasserdin Nabi ambaye kwasasa ameweka wazi hayupo tayari kupokea Ofa mpya nje ya Yanga SC.

Wakati tetesi hizo zikizidi kushika kasi huko Sudan, Sokahubtz wamefatilia kwa undani na kugundua kwamba Al Hilal Omdurman wenyewe hawana mpango wa kumwacha Ibengè aondoke kwani wanataka aendelee kusalia ndani ya timu hiyo kwaajili wana mpango na Ibenge wa muda mrefu lakini hali ya Sudan kwa sasa inaweza kufanya mambo kuwa magumu kumbakisha.

SOMA NA HII  MZEE WA KUCHETUA, MORRISON HANA BAHATI NA YANGA, SABABU HIZI HAPA