Home Habari za michezo USHINDI ZIDI YA WAARABU WAIONGEZA YANGA JEURI…WATANGAZA KUSEPA NA KILA KITU…

USHINDI ZIDI YA WAARABU WAIONGEZA YANGA JEURI…WATANGAZA KUSEPA NA KILA KITU…

Habari za Yanga

Uongozi wa Yanga SC, umeweka wazi kuwa, akili zao zinafikiria kupata mafanikio kwenye kila mashindano wanayoshiriki kwa kubeba ubingwa.

Yanga ni mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Bara ambapo walisepa nalo msimu uliopita kutoka mikononi mwa watani zao wa jadi Simba.

Ally Kamwe ambaye ni Ofisa Habari wa Yanga, alisema: “Kwenye mashindano ambayo tunashiriki yote akili zetu ni kuona tunashinda ubingwa, hilo lipo wazi.

“Hakuna namna, ushindani kwenye ligi ni mgumu na wachezaji wanalijua hilo, hivyo ambacho tunakifanya ni kupata matokeo mazuri, hilo litafanyika mpaka mwisho wa msimu.”

Baada ya kucheza mechi 8 za Ligi Kuu Bara, Yanga imefikisha pointi 20, ipo kileleni mwa msimamo kabla ya mechi za juzi Jumatano.

Timu hiyo ambayo juzi ilicheza dhidi ya Club Africain katika kuwania kutinga makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika, msimu huu tayari imebeba Ngao ya Jamii kwa kuifunga Simba mabao 2-1.

SOMA NA HII  OKRAH AFUNGUKA KILICHOMVUTA YANGA....AMTAJA 'MBAYA WA SIMBA'....